Thobias Minzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Thobias Minzi alizaliwa mwaka 1984 huko jijini Mwanza. [1]Alizaliwa katika kijiji cha Iseni katika wilaya ya Mwanza huko kaskakazini mwa Tanzania.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Minzi alianza shule ya msingi mnamo mwaka 1994 katika shule ya msingi Iseni. Mwaka 2000, Minzi alifanikiwa kuhitimu elimu ya msingi.[2]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Pindi alipohitimu shule ya msingi, Minzi alisafiri kutokea jijini Mwanza kuelekea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Sanaa ya uchoraji. Mnamo mwaka 2002, Minzi alijiunga na kundi la wapaka rangi liitwalo Namanga Art Studio. [3]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Minzi ni mchoraji na mchukua filamu. Aliweza kutengeneza namna ya kisanaa ya kutumia uzi na nguo kufikisha picha na hisia. Michoro ya Minzi inaonyesha wanawake na watoto, majukumu wanayoyafanya katika Maisha ya kila siku ya kiafrika pamoja na changamoto wanazozikumba na kukabiliana nazo katika nchi zinazoendelea. [4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Thobias Minzi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.