The Joplin Globe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
The Joplin Globe
Jina la gazeti The Joplin Globe
Aina ya gazeti Gazeti la kila siku
Lilianzishwa 1896
Nchi Marekani Marekani
Mwanzilishi Thomas G. Barbee
Mmiliki Kampuni ya Magazeti ya Community (CNC)
Mchapishaji Dan Chiodo
Makao Makuu ya kampuni * 117 East Fourth Street
* Joplin
* Missouri 64801
Nakala zinazosambazwa 30,558 kila siku
Tovuti http://www.joplinglobe.com

Historia[hariri | hariri chanzo]

The Joplin Globe ni gazeti la kuchapishwa kila siku kwa wiki katika eneo la Joplin, Missouri,Marekani. Linasambazwa katika makata 14 katika kusinimashariki mwa Missouri. Tangu mwaka wa 2002, imemilikiwa na shirika la Community Newspaper Holdings.

Gazeti hili linaajiri wanahabari 45 katika chumba chake cha habari. Kaulimbiu yake ya masoko ni "Ni dunia yako. Sisi tunawasilisha tu." [1]

Habari ya Bonnie na Clyde[hariri | hariri chanzo]

Katika mwaka wa 1933, The Joplin Globe ilipata habari muhimu sana ya kitaifa baada ya kupata kamera iliyoachwa nyuma na Bonnie na Clyde. Baada ya mapambano na polisi wa mtaa, walichapisha picha zilizotolewa kutoka filamu ya kamera hiyo. Picha hizi ni kama zile maarufu za Bonnie akimshika Clyde na kuigiza kuwa amemshikia Clyde bastola na za Bonnie akiwa akiwa ameshika bastola mkononi mmoja na sigara mdomoni mwake.

Mwanzilishi[hariri | hariri chanzo]

Thomas G. Barbee alizaliwa katika mwezi wa Oktoba 1870 katika Ritchey, katika kata la Newton, Missouri. Thomas alimwoa Laura (jina lake la pili halijulikani) aliyekuwa amezaliwa Januari 1874 katika Missouri. Barbee alimiliki Joplin Globe na akaanzisha kuchapisha gazeti la Joplin Tribune. Barbee alifariki tarehe 18 Oktoba 1924 katika Joplin, kata la Jasper, Missouri.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^ CNHI-CAN Circulation, figures for an undetermined date,.
  2. ^ Joplin Globe FAQ, .
  3. ^ Court TV, CrimeLab website, ukurasa wa Bonnie na Clyde.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]