Nenda kwa yaliyomo

Tamasha la Ngmayem

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tamasha la Ngmayem ni tamasha la mavuno la kila mwaka linaloadhimishwa na machifu na watu wa Manya Krobo katika Mkoa wa Mashariki wa Ghana. Tamasha hili lilianzishwa na Nene Azu Mate Kole mnamo mwaka 1944[1] kurekebisha tamasha lililokuwepo awali linaloitwa Yeliyem, ambalo kwa tafsiri ya moja kwa moja linamaanisha kula mtama.Kawaida huadhimishwa katika mwezi wa Oktoba huko Dodowa na pia katika maeneo ya Shai kwenye miji ya Somanya na Odumase.[2] Tamasha hili huadhimishwa kwa wiki moja, hasa kutoka Jumapili za mwisho mbili za mwezi wa Oktoba.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "The Manya Krobo Annual Ngmayem Festival". Modern Ghana (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-10-18.
  2. "Festival | The Embassy of the Republic of Ghana, Berlin, Germany" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-08-16.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tamasha la Ngmayem kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.