Nenda kwa yaliyomo

Tamasha la Gmayem

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tamasha la Gmayem pia linajulikana kama tamasha la Mgmayem, linaadhimishwa na machifu na watu wa Wilaya ya Shai Osudoku ya Ghana.[1] Tamasha la Mgmayem hufanyika kila mwaka na huwaleta pamoja wananchi wa eneo hilo, walioko nyumbani na wale waishio nje, kupanga njia za kuleta maendeleo. Tamasha hili pia hufanyika kwa kumbukumbu ya kumalizika kwa njaa iliyowaathiri watu karne nyingi zilizopita. Kwa wakati huu kwenye kalenda ya eneo la jadi, mazishi yote husimamishwa hadi tamasha litakapomalizika na watu wanahimizwa kuheshimu mpango huo na adhabu kali inamsubiri yeyote atakayekiuka agizo hilo.[2] Inasemekana tamasha hili huadhimishwa mwezi wa Oktoba kila mwaka lakini hubadilika kulingana na kalenda yao ya jadi.[1]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "Festivals in Ghana". www.ghanaweb.com. Iliwekwa mnamo 27 Desemba 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Allow Chiefs To Take Part In Partisan Politics". The Ghana Star (kwa American English). 2016-09-07. Iliwekwa mnamo 2020-03-27.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tamasha la Gmayem kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.