Sun Tzu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sun Tzu
(pia: Sūn Zǐ)
Jina la kuzaliwa Sun Wu
Alizaliwa mnamo 500 KK
Nchi China
Kazi yake Jenerali, mwandishi,
mwanafalsafa

Sun Tzu aliyeishi manmo mwaka 500 KK alikuwa jenerali, mwandishi na mwanafalsafa kutoka nchini China.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Hakuna mengi yanayojulikana juu yake. Aliitwa Sun Wu akapewa jina la Sun Tzu kwa heshima na "Tzu" ilimaanisha "mwalimu".

Alikuwa jemadari wa mfalme Helü katika ufalme Wu uliokuwepo kwenye mto Yangtse karibu na mdomo wake.

Kuna hadithi juu yake ya kwamba siku moja mfalme alimwamuru kuonyesha utaalamu wake kama jenerali. Akampa hawara 300 wa nyumba yake. Sun Tzu aliwagawa katika vikosi viwili akaweka hawara 2 waliopendwa hasa na mfalme kama maafisa. Baadaye aliwaeleza amri kadhaa akawapa amri watekeleze. Hawara walianza kucheka tu bila kufanya kitu. Sun Tzu alisema: "Kama amri si dhahiri na askari hawaelewi ni kosa la jenerali" akaeleza shughuli tena na kurudia amri. Mabinti walicheka tena. Sasa alisema: "Kama amri zinaeleweka na askari hawatii ni kosa la maafisa" akatoa amri ya kukata vichwa vya hawara 2 waliopendwa na mfalme. Baada ya kuona vifo vya wenzao wengine walitii bila kusita tena.

Mfalme aliyeshtuka mwanzoni aliona huyu anafaa kuwa jenerali alimfanya jemadari wa ufalme.


Mafundisho[hariri | hariri chanzo]

Kitabu chaSanaa ya Vita kilichoandikwa kwenye mwanzi

Aliandika kitabu "Sanaa ya Vita" kinachosomwa hadi leo anamoeleza nadharia ya vita.

Mafundisho yake ni ya kwamba vita ni jambo la hatari ni afadhali kuepukana nayo ka sababu mara nyingi inaharibu taifa na dola. Vita inapaswa kufuata shabaha ya siasa inayoeleweka na kumaliza baada ya kufika shabaha.

Alisema ni bora kuvurugisha mipango ya adui kuliko kupambana naye, halau ni afadhali kuvunja ushikamano wake na wasaidizi na kwenye nafasi ya tatu tu ni kuingia vitani na kushinda.

Athira[hariri | hariri chanzo]

Kitabu cha Sun Tzu inasomwa na kufundishwa hadi leo katika vyuo vya kijeshi mbalimbali. Kati ya viuongozi wa kijeshi waliotafakari ushauri wa kitabu hii ni

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: