Sudusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sudusi ni sehemu ya sita ya jumla fulani. Neno limepokelewa katika Kiswahili kutoka Kiarabu ambako linaitwa سُدْس suds. Inaweza kuandikwa pia au 1/6. Ikiandikwa kwa namna ya kidesimali ni 0.166666666666667.

Katika familia ya Waislamu sudusi inataja sehemu ya urithi inayopokelewa na mama wa marehemu.

Mabaharia walitumia kifaa kinachoitwa Sudusi (ing. sextant) kwa kupima pembe za Jua na nyota baharini na hivyo wakiweza kukadiria mahali pao baharini.