Stories Of Change
Stories Of Change ni shindano la uandishi linalofanyika kila mwaka nchini Tanzania linaloratibiwa na taasisi na asasi ya kiraia ya Jamii Forums.[1]
Shindano hili lilianzishwa kwa lengo la kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani yenye lugha ya Kiswahili lakini pia kuhamasisha ushiriki wa makundi yasiyopewa vipaumbele kama vile walemavu katika uboreshaji wa mambo mbalimbali nchini Tanzania[2].[3]
Mshindi wa Stories Of Change hupokea zawadi ya pesa taslim ambapo kwa mwaka 2021 na 2022 mshindi alipokea Milioni 5 na 2023 mshindi alipata Tsh Milioni 7.[4]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Shindano La Stories Of Change lilianza rasmi mwaka 2021. Kulingana na mkurugenzi wa Jamii Forums, Maxence Melo alidokeza kuwa alianzisha shindano hilo ili kuweza kuchochea mabadiliko katika jamii hasa kwenye nyanja za Utawala bora, Uchumi, Uwajibikaji, Afya, Kilimo, Sayansi na Teknolojia.[5]
Mwaka 2022, shindano hilo lilirudi tena kwa ushirikiano na Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa umma, Chuo kikuu cha Dar es Salaam SJMC na muungano wa Klabu za Waandishi wa habari ( UTPC) ambapo shindano lilianza rasmi Julai 15 na kumalizika rasmi Septemba 14. [6]
Kwa mwaka 2022, takriban wananchi 1509 walishiriki kwenye shindano hilo ambapo walishriki kuandika machapisho takriban 1539.[7]
Mwezi Mei mwaka 2023 Jamii Forums walizindua msimu tatu wa Stories Of Change takribani maandiko 1,778 yaliletwa kwa ajili ya kuchapishwa ambapo kati ya hao machapisho takriban 1,224 yalikidhi vigezo vya kuchapishwa.[8]
Kilele cha msimu wa 3 yalifanyika mwezi Septemba kwenye hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar Es Salaam.[9]
Vigezo vya Ushiriki
[hariri | hariri chanzo]Miongoni mwa vigezo na masharti vya kushiriki kwenye Stories Of Change ni lazima mshiriki awe amejisajili katika Jukwaa la JamiiForums.com[10]
Pia, andiko libebe maono ya mwaka husika na maono yawe na uwezo wa kutekelezeka kwa Miaka 5-25 ijayo.
Andiko liwe na Maneno yasiyopungua 700 na yasiyozidi 1,000 kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza.
Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha ( thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%)
Zawadi na Washindi
[hariri | hariri chanzo]Kwa mwaka 2021, Golder Mmari aliibuka mshindi wa kwanza ambapo alijinyakulia kitita cha Tsh Milioni 5 akifuatiwa na Shiija Masele ambaye alikuwa ni mshindi wa pili.
Mshindi wa 2022 alikuwa ni Kulwa Masanja Isenge ambaye aliondoka na kitita cha Tsh Milioni 5 akifuatiwa na Jayson Mkelame ambaye aliondoka na Tsh Milioni 3[11]
Mwaka 2023, alishinda Athanas Mnyonga kiasi cha Tsh Milioni 7 akifuatiwa na Respick Tairo Hugolini ambaye alishinda Milioni 4.[12]
Aidha, maandiko ya washindi hupelekwa kwa mamlaka zinazohusika kwa ajili ya tathmini na utekelezaji.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Stories of Change". JamiiForums (kwa American English). 2024-09-20. Iliwekwa mnamo 2024-09-20.
- ↑ Michuzi Blog. "JAMII FORUMS YAZINDUA AWAMU YA PILI YA SHINDANO LA 'STORIES OF CHANGE'". MICHUZI BLOG. Iliwekwa mnamo 2024-09-19.
- ↑ "Tsh Milioni 50 kushindaniwa shindano la Uandishi "Stories of Change" – Bongo5.com". bongo5.com. Iliwekwa mnamo 2024-09-19.
- ↑ joseph (2022-07-13). "JAMII FORUMS YAZINDUA AWAMU YA PILI YA SHINDANO LA " STORIES OF CHANGE"". Full Shangwe Blog (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-09-19.
- ↑ "From arrests to milestones: Maxence Melo's stand for data privacy in Tanzania". The Citizen (kwa Kiingereza). 2024-09-15. Iliwekwa mnamo 2024-09-19.
- ↑ AjiraLeo Tanzania. "JamiiForums Stories of Change Competition (Award Cash 10 Tsh Million & Electronics Device) | Apply Now". AjiraLeo Tanzania. Iliwekwa mnamo 2024-09-19.
- ↑ "JamiiForums waungana na SJMC, UTPC shindano uandishi bora wa makala". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2022-07-13. Iliwekwa mnamo 2024-09-19.
- ↑ Habari Mseto. "JamiiForums yazindua Awamu ya Nne Shidano la Stories of Change, Wananchi wahamasishwa kushiriki kuibua Mawazo". HABARI MSETO BLOG. Iliwekwa mnamo 2024-09-19.
- ↑ Michuzi Blog. "JAMII FORUMS YAZINDUA AWAMU YA PILI YA SHINDANO LA 'STORIES OF CHANGE'". MICHUZI BLOG. Iliwekwa mnamo 2024-09-19.
- ↑ "Uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Shindano la Stories of Change(2022)". JamiiForums (kwa American English). 2022-07-13. Iliwekwa mnamo 2024-09-19.
- ↑ "Kulwa Masanja Isenge anyakua milioni 5 katika Shindano la 'Stories of change' 2022". JamiiForums (kwa American English). 2022-11-18. Iliwekwa mnamo 2024-09-19.
- ↑ "Athanas Myonga Ashinda Tsh. Milioni 7 za Shindano la Stories Of Change 2023". Global Publishers (kwa American English). 2023-10-08. Iliwekwa mnamo 2024-09-19.