Nenda kwa yaliyomo

Steven Gardiner

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gardiner kwenye Mashindano ya Dunia ya 2019
Gardiner kwenye Mashindano ya Dunia ya 2019

Steven Gardiner (alizaliwa 12 Septemba 1995)[1] ni mkimbiaji wa mbio fupi kutoka Bahamas akishindana katika mita 400 na mita 200.  Kwa sasa ni Bingwa wa Olimpiki na Dunia katika mita 400, na alishinda medali ya fedha kwenye Mashindano ya Ubingwa wa Dunia mwaka 2017 kwenye mbio hizo.[2] Muda wake alioshindia wa sekunde 43.48 kwenye Mashindano ya Ubingwa wa Dunia mwaka 2019 ni rekodi ya Bahamas na inamfanya awe nafasi ya sita kwa watu wenye kasi zaidi katika historia ya mbio hizo.[3] Gardiner pia anashikilia rekodi ya Bahamas kwenye mita 300 na mita 200, kwa muda wa sekunde 31.83 na sekunde 19.75 kwa mpangilio huo.

  1. https://olympics.com/en/athletes/steven-gardiner
  2. "Gardiner powers away to win dramatic 400 meters", Reuters (kwa Kiingereza), 2019-10-04, iliwekwa mnamo 2021-10-16
  3. "400 Metres - men - senior - outdoor". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-16.