StarCraft
StarCraft ni mchezo wa video unaohusu sayansi ya kijeshi na mikakati uliotengenezwa na Blizzard Entertainment.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Mchezo wa kwanza wa mfululizo StarCraft ulitolewa kwa Microsoft Windows tarehe 31 Machi 1998. Na zaidi ya nakala milioni 11 kuuzwa duniani kote kufikia Februari 2009, ni moja ya michezo bora kwa kuuza inayotumika kwenye kompyuta binafsi. Nakala inayotumika kwenye Mac OS ilitolewa Machi 1999.
Vitimbi
[hariri | hariri chanzo]Mchezo huu unatokea katika karne ya 26, mchezo unahusisha aina tatu ya viumbe vinavyopambana kupata utawala katika sehemu mbali kwenye anga za mbali: Terrans,ambao ni binadamu walitoroka kutoka Dunia na wenye ujuzi wa kuishi katika hali yoyote; Zerg, ambao ni viumbe wanaofanana na wadudu wako katika harakati za maumbile ukamilifu na ukoloni wa jamii nyingine; na Protoss,ambao ni viumbe wanaofanana na binadamu lakini wana ujuzi wa kiteknolojia na uwezo wa psionic wanajaribu kuhifadhi ustaarabu wao na njia ya falsafa kali ambayo hailingani na ile ya Zerg. Mchezo huu umesifiwa kwa kuanzisha mtindo wa matumizi ya makundi ya kipekee katika michezo ya mikakati na kwa hadithi yenye kusisimua.
Wengi wa waandishi wa habari katika sekta hii wameisifu StarCraft kama mojawapo ya michezo bora na muhimu kabisa, na kwa kuongeza kiwango cha uzuri wa michezo ya mikakati. Mbinu ya kucheza StarCraft inayohusisha wachezaji wengi ni maarufu hasa katika Korea ya Kusini, ambapo wachezaji wenye umaarufu na timu hushiriki katika mechi,hufadhiliwa na makampuni, na kushindana katika mashindano yanayotangazwa.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Official StarCraft website
- The StarCraft Compendium on Battle.net Ilihifadhiwa 25 Februari 2011 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu StarCraft kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |