Nenda kwa yaliyomo

Soko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
soko
Soko la kisasa huko Singapore.

Soko ni sehemu ambapo watu huuza na kununua bidhaa. Wakati watu wana bidhaa za kuuza, huanzisha mahali pa kuuzia, inaweza kuwa sehemu maalum.

Neno "soko" linaweza likajumuisha maana kwenye uchumi. Linaweza kumaanisha njia ambayo bidhaa zinauzwa na kununuliwa. "Kuna masoko makubwa kwa ajili ya maosheo ya vyombo" ina maana watu wengi wananunua maosheo ya vyombo. Kwa hiyo biashara ya maosheo ya vyombo inaweza kuingiza pesa nyingi. Na hii huchochea uchumi.

Soko ni mahali muhimu kwa kuwa inao watu wengi. Huenda wakawa wengi sana kama milioni. Kuna aina ya masoko ya watu wengi ndani ya nchi za Afrika, kwa mfano Cairo, Lagos, Kinshasa, Soweto (Johannesburg).

Ushindani

[hariri | hariri chanzo]

Kama muuzaji wa bidhaa hawezi kusambaza kile ambacho mteja anaulizia au anataka kwa bei ndogo, wauzaji wengine wanaweza wakasambaza kwa bei ndogo. Wauzaji huwa hawapendi ushindani na wanaweza kujaribu kuua ushindani. Muuzaji anayeua ushindani kwa ajili ya yeye kupata faida hambazo hakutakiwa kupata, anatakiwa kusimamishwa kisheria.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Soko kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.