Sheila Meiring Fugard

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sheila Meiring Fugard (alizaliwa Birmingham, England, mwaka 1932) alihamia na wazazi wake Afrika Kusini mwaka 1940 alipokuwa na miaka nane. Alikwenda Chuo Kikuu cha Cape Town, ambapo aliandika hadithi fupi na kusoma ukumbi wa michezo. Alikutana na mwandishi wa michezo Athol Fugard wakati akiwa anacheza katika moja ya michezo yake. Mnamo Septemba 1956, aliolewa na Fugard na kuchukua jina lake la ukoo..[1]

Mnamo 1972, alipokuwa na umri wa miaka 40, Sheila Fugard alichapisha riwaya yake ya kwanza iitwayo, The Castaways,ambayo ilishinda Tuzo ya Olive Schreiner,Baadaye, mnamo mwaka 1976 alichapisha riwaya nyingine iitwayo "Rite of Passage", na "Mwanamke wa Mapinduzi", mnamo 1983."Mwanamke wa Mapinduzi", riwaya yake iliyojulikana zaidi katika miaka ya 1920 uko Karoo wilaya ya Afrika Kusini na inasimulia hadithi ya mwanafunzi wa kike wa Mahatma Gandhi,ambaye alivutiwa na kesi ya ubakaji kati ya mvulana wa rangi na msichana mdogo wa Boer. Fugard pia amechapisha mashairi kama Threshold, in 1975, and Mystic Things, in 1981. Athol Fugard aligiza katika marekebisho ya BBC ya riwaya yake ya "The Castaways". Binti yao, Lisa Fugard, ambaye ameigiza katika baadhi ya michezo ya baba yake, kama vile My Children! My Africa!”, Ameandika pia riwaya.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Riwaya
  • The Castaways (1972). ISBN|0-333-14222-5.
  • Rite of Passage (1976). ISBN|0-86068-620-5.
  • A Revolutionary Woman (1983). ISBN|0-86068-620-5.
Shairi
  • Threshold (1975). ISBN|0-949937-11-8.
  • Mystic Things (1981). ISBN|0-949937-87-8.
  • The Magic Scattering Of A Life (2006). ISBN|0-9535058-4-7.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

  1. Craig McLuckie (Okanagan College) (2003-10-08). "Athol Fugard (1932–)". The Literary Encyclopedia. Iliwekwa mnamo 2008-09-29.