Shamba la miti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
miti

Shamba la miti/msitu linaweza kuanzishwa kwa kupanda miche au mbegu moja kwa moja. Utumiaji wa mbegu moja kwa moja sio Jambo la kawaida ila inawezeka iwapo mbegu husika ni kubwa (mbegu zenye urefu usiopungua sentimeta (SM) 1 au zisizozidi 8,000 kwa kilo moja) na uotaji wake usiopugua asilimia 75 ambao unakamilika kabla ya siku 14 tangu zipandwe ardhini. Ili miche mingi iliyopandwa iweze kupona na kustawi vyema, inabidi kufanya yafutavyo:

  • Kuoanisha aina ya miti na mahali pa kupanda;
  • Kutayarisha au kutifua ardhi vizuri ili kusaidia mizizi kupenya kwa urahisi na kunyonya virutubisho;
  • Kudhibiti magugu;
  • Kuchimba mashimo yenye Kina na upana unaostahili;
  • Kuacha nafasi inayostahili kati ya miti na miti;
  • Kuweka mbolea pale inapostahili.

Kupanda miti kujulikane kabla ya kupanda. Kuchagua aina ya miti ya kupanda na umbali kati ya miti vitategemea matumizi yanayokusudiwa wakati miti Itakapovunwa. Madhumuni yanaweza yakawa ni kupata nishati (Kuni, mkaa au vyote), Mbao nguzo, kivuli, mapambo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]