Shajara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shajara ya kale mwaka 1787

Shajara (kwa lugha ya Kiingereza: diary) ni kitabu maalumu ambamo mwandishi huandika matukio ya kila siku au ya muda fulani.

Shajara ya kibinafsi huenda ikawa na mawazo ya mwandishi; yaliyompata kwa siku na maazimio yake ya siku zijazo.

Kando na shajara ya kibinafsi, kuna shajara rasmi kama za mashirika ("Logbook") ambazo huonyesha matukio ya shirika hilo. Aidha, kabla ya wanafunzi kuhitimu katika kozi zao, wao huenda kwa Kiambatisho Cha Viwanda (Industrial Attachment) na wanahitajika kuandika matukio ya kila siku kwa muda wa miezi mitatu hivi katika Shajara.

Wahasibu pia huwa na shajara ambamo hurekodi kiwango cha pesa walizotumia kununua vitu au zile ambazo zimeingia kwa shirika.