Senegermini
Senegermini (Cenegermin), inayouzwa kwa jina la chapa Oxervate, ni dawa inayotumika kutibu keratiti ya neva, yaani, ugonjwa utokanao na kuzorota kwa konea unaosababishwa na kuharibika kwa neva ya trijeminali (trigeminal nerve).[1] Inatumika kwa wale walio na ugonjwa wa wastani au mkali.[1] Matumizi yake hayakupendekezwa na Uingereza.[2] Dawa hii inatumika kama tone la jicho.[3]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya macho, kuongezeka kwa machozi, na maumivu ya kope.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[2] Ni aina ya mchanganyiko tena wa sababu ya ukuaji wa neva.[2]
Senegermini iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu barani Ulaya mnamo 2017 na Amerika mnamo 2018.[1][3] Nchini Marekani, vichupa 14 hugharimu takriban dola 23,600 kufikia mwaka wa 2021.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "Oxervate". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 31 Oktoba 2020. Iliwekwa mnamo 2 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1210. ISBN 978-0857114105.
- ↑ 3.0 3.1 "Cenegermin-bkbj Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 2 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Oxervate Prices and Oxervate Coupons - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 2 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Senegermini kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |