Nenda kwa yaliyomo

Secukinumab

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Secukinumab, inayouzwa kwa jina la chapa Cosentyx, ni dawa inayotumika kutibu psoriasis (yaani ugonjwa wa ngozi ambao husababisha mabaka mekundu, kavu, na yenye ngozi iliyovimba), arthritis ya muda mrefu inayosababisha maumivu na kuvimba hasa kwenye uti wa mgongo (spondylitis ankylosing), na ugonjwa wa viungo unaoambatana na psoriasis (psoriatic arthritis).[1] Dawa hii inatolewa kwa njia ya kudungwa sindano chini ya ngozi.[2]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na mafua ya pua, kuhara, vidonda vya baridi na upele wa ngozi unaosababishwa na mwitikio dhidi ya chakula, dawa, au vitu vingine vinavyokereketa.[2] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha mshtuko wa mzio mkal (anaphylaxis) na maambukizi.[2] Dawa hii haipendekezwi kutumiwa wakati wa ujauzito au kunyonyesha.[3] Ni kingamwili ya monokloni inayojifunga na kuzuia interleukin (IL)-17A (aina ya protini ya kuashiria ya kinga inayozalishwa na chembechembe za kinga, hasa seli za T).[2]

Secukinumab iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani na Ulaya mwaka wa 2015.[2][1] Nchini Uingereza, miligramu 150 hugharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban £600 kufikia mwaka wa 2021.[3] Kiasi hiki nchini Marekani kinagharimu takriban dola 6,200 za Kimarekani.[4]

  1. 1.0 1.1 "Cosentyx". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 11 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 "Secukinumab Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 11 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 BNF (tol. la 80). BMJ Group and the Pharmaceutical Press. Septemba 2020 – Machi 2021. uk. 1162. ISBN 978-0-85711-369-6.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: date format (link)
  4. "Cosentyx Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Juni 2021. Iliwekwa mnamo 11 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Secukinumab kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.