Scientific Detective Monthly

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ukurasa wa mbele wa toleo la pili; mchoro na Jno Ruger.

Scientific Detective Monthly (linajulikana pia kama Amazing Detective Tales na Amazing Detective Stories) lilikuwa na gazeti lililotolewa kwa matoleo 15 kuanzia Januari 1930. Lilianzishwa na Hugo Gernsback kama mradi wake wa pili wa uchapishaji wa riwaya za kisayansi likiwa na nia ya kulenga habari za upelelezi zenye maudhui ya kisayansi.

Jina lake lilibadilishwa na kuitwa Amazing Detective Tales katika toleo lake ha Juni 1930, pengine kuepuka kutumia neno "scientific" kwani ingeweza kuwafanya wasomaji wadhani kuwa ni jarida la kisayansi. Wakati huo huo mhariri wake—Hector Grey—alibadilishwa na David Lasser ambaye alikuwa tayari anahariri magazeti mengine ya Gernsback. Hata hivyo kubadilishwa kwa jina lake hakukusaidi kuleta mafanikio ya gazeti na Gernsback akalifunga gazeti baada ya toleo la Octoba. Aliliuza gazeti hilo kwa mchapishaji Wallace Bamber ambaye alichapisha matoleo matano kwa jina la Amazing Detective Stories hadi mwaka 1931.