Rosa Parks

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rosa Parks wakati alipokamatwa kwa kosa la kutomwachia kiti chake Mwamerika Mzungu

Rosa Louise McCauley Parks (4 Februari 191324 Oktoba 2005) anakumbukwa kwa uamuzi wake wa kukataa kumpisha kiti Mmarekani mweupe kama alivyodaiwa na dereva wa basi. Uamuzi wake huo hapo mwaka 1955 ulipelekea mzozo uliosababisha Mgomo wa Mabasi wa Montgomery na kuchangia katika Vuguvugu la Haki za Kiraia Marekani. Baada ya kitendo chake cha kukataa kumpa mtu mweupe kiti ndani ya basi na Mgomo wa Montgomery uliodumu kwa mwaka, Mahakama ya Marekani ilitamka kuwa sheria za ubaguzi ndani ya mabasi huko Alabama na Montgomery zilikiuka katiba.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]