Robert James Waller

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Robert James Waller (Rockford, Iowa 1 Agosti 1939 - 10 Machi 2017) alikuwa mwandishi wa vitabu wa Marekani, pia anafahamika kwa kazi zake za upigaji picha na uanamuziki.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Waller alipokea shahada yake ya kwanza kutoka katika chuo kikuu cha Noth Lowa kilichofahamika kama University of Northern Iowa, kwa wakati huo kilikua kikifahamika kama (Lowa state Teachers College) [1] . Baadae, alipata stashahada ya udaktari katika biashara kutoka shule ya biashara ya Kelley School of Business iliyopo katika chuo kikuu cha Indiana University Bloomington, hii ikiwa ni mnamo mwaka 1968 Katika miaka iliyofuatia alirejea UNI na kuanza kazi ya kufundisha katika shule za uongozi na uchumi na mwaka 1977 aliweza kutunukiwa rasmi nishani ya Uprofesa. Na baadae aliweza kuwa mshauri wa wanafunzi katika katika College of Business hii ikiwa ni mwaka 1980, na aliweza kustaafu kazi hiyo mwka 1986. [2] Vitabu vyake kadhaa vimeweza kuchapishwa katika magazeti ya New York Times, ikiwa ni pamoja na kile cha The Bridges of Madison County mwaka 1992, ambacho kiliongoza kwa mauzo kwa mwaka 1993. Kitabu cha The Bridges of Modison Country na kingine kilichotoka mwaka 1995, kilichofahamika kwa jina la Puerto Vallarta Squeese viliweza kutengenezea na kuigizwa katika filamu. Kwa sasa Waller anakaa Texas

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Riwaya[hariri | hariri chanzo]

Makusanyo[hariri | hariri chanzo]

  • Just Beyond the Firelight (1988)

Isiyo ya kuigiza[hariri | hariri chanzo]

  • One Good Road is Enough (1990)
  • Iowa: Perspectives on Today and Tomorrow (1991)
  • Old Songs in a New Café (1994)
  • Images (1994) [3]

Muziki[hariri | hariri chanzo]

  • The Ballads of Madison County: A Collection of Songs

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Famous UNI Alumni". Rod Library, University of Northern Iowa. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-08. Iliwekwa mnamo 17 Mei 2011. 
  2. "Author Waller leaves large estate gift to alma mater". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-09-01. Iliwekwa mnamo 2011-12-13. 
  3. "Images". amazon. Iliwekwa mnamo 17 Mei 2011.