Nenda kwa yaliyomo

Rifamisini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rifamisini

Rifamisini, yaani Rifamycin, inayouzwa chini ya jina la chapa Aemcolo, ni dawa ya kukinga inayotumika kutibu kuhara kwa wasafiri.[1] Haipendekezwi kuitumia ikiwa mtu ana homa au kinyesi chenye damu.[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya kichwa na kuvimbiwa choo.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kuhara kunakohusishwa na Clostridium difficile.[2] Usalama wa mayumizi yake katika ujauzito na kunyonyesha hauko wazi.[3] Dawa hii ni katika kundi la dawa za rifamisini (rifamycins).[1]

Rifamisini iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mnamo mwaka wa 2018.[1] Nchini Marekani, mzunguko wa matibabu yake unarudiwa uligharimu takriban dola 190 kufikia 2021.[4]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Rifamycin Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "DailyMed - AEMCOLO- rifamycin tablet, delayed release". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Rifamycin (Aemcolo) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Aprili 2021. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Aemcolo Prices and Aemcolo Coupons - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rifamisini kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

>