Rare (conservation organization)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Rare ni asasi isiyolenga faida ya kidunia inayojihusisha na Mazingira yenye dira ya kuhamasisha mabadiliko kwa watu na mazingira ya asili. Makao makuu ya asasi hii ni Nchini Marekani, Rare, ina mipango na watumishi katika Nchi zaidi ya 10 (ikijumuisha nchi za Ufilipino, Indonesia, Msumbiji, Brazil, Visiwa vya Pasifiki, Ukanda wa Mesoamerican, na Ujerumani). Inafanya kazi za ulinzi wa baoanuai, kuboresha Maisha, usawa wa kijinsia, na usalama wa chakula, na kuifanya jamii na Nchi zaidi kuhimili mabadiliko. Rare imewawezesha zaidi wa watu milioni 10,kupitia zaidi ya kampeni 450 za mabadiiko ya tabia, kuwabadilisha tabia zao na matendo ili kuilinda dunia tuliyonayo. [1]

Rare ilipokea heshima ya nyota 4 kati ya 4 kutoka Charity Navigator.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Bobrow, Emily (2 June 2017). "Conservation That Works for Locals". The Wall Street Journal. Iliwekwa mnamo 18 November 2018.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. "Charity Navigator Rating – Rare". Charity Navigator. Iliwekwa mnamo 2021-11-10.