Nenda kwa yaliyomo

Pramlintidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pramlintidi (Pramlintide), inayouzwa chini ya jina la chapa Symlin, ni dawa inayotumika kutibu kisukari cha aina ya 1 na 2 kwa watu wanaotumia insulini wakati wa chakula.[1] Inatolewa kwa kudungwa sindano chini ya ngozi.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, kupoteza hamu ya kula na maumivu ya kichwa.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha sukari ya chini ya damu na athari za mzio. [1][2] Haipendekezwi kuitumia kwa watu wenye hali inayoathiri misuli ya tumbo na kuzuia kutoa vizuri vilivyomo tumboni (gastroparesis).[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[3] Ni analogi ya amilini (amylin).[1]

Pramlintidi iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2005.[1] Nchini Marekani, dozi 50 za mikrogramu 60 hugharimu takriban dola 1,000 kufikia mwaka wa 2021.[4]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "DailyMed - SYMLINPEN- pramlintide acetate injection". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Pramlintide Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Pramlintide Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "SymlinPen 60 Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pramlintidi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.