PinkPantheress

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pinkpantheress ni mwimbaji wa Uingereza lake hasili ni Victoria Beverley Walker. Ana umri wa miaka 20. Alijipatia umaarufu mkubwa sana katika mwaka wa 2021 kwa sababu ya wimbo wake “Just for Me” ambao ulipata umaarufu mkubwa kwenye programu ya TikTok. Tangu wimbo huo kutolewa amekuwa mwimbaji maarufu sana wa muziki wa pop.

Maisha binafsi na historia[hariri | hariri chanzo]

Foto ya PinkPantheress

PinkPantheress anatoka mjini Bath mkoa wa Somerset nchini Uingereza na alizaliwa mwaka wa 2001. Mama yake ni Mkenya na baba yake ni Mwingereza. Mama yake ni MLuo na yeye anatoka mji wa Kisumu nchini Kenya. Ana kaka mkubwa mmoja. Alipokuwa na miaka kumi na mbili, baba yake alihamia jimbo la Texas nchini Marekani kufanya kazi kama mwalimu wa takwimu. Familia nzima ilikuwa inatarajiwa kuhamia pamoja naye, lakini PinkPantheress aliaua kubaki shueni kwake na kwa marafiki zake. Hii ilikuwa na athari kubwa kwa mtindo wake wa muziki.[1]

Amekuwa akipenda muziki tangu utotoni mwake. Wazazi wake walimfundisha kuhusu aina za muziki mbalibali kama vile muziki wa Michael Jackson (muziki wa Pop), muziki wa Queen (muziki wa Rock), na muziki wa Kiafrika. Kaka yake ni mhandisi wa sauti na alikuwa akimpeleka kwenye maonyesho ya muziki huko London. Alisomea utando katika Chuo Kikuu cha Sanaa mjini London hadi mwaka wa 2022.

Ameelezea kupitia kwamba amekuwa kuhusu akisumbuliwa dysmorfia ya mwili tangu utotoni, akisema kuwa hali hiyo imekuwa ikizidi kuwa mbaya kadri alivyozidi maarufu.[2] Pia alipoteza uwezo wa kusikia kwa asilimia themanini katika sikio lake la kushoto kwa sababu ya kusikiliza sauti kubwa sana na mwitikio wa mara kwa mara wa mikrofoni.[3]

Sasa, licha ya umaarufu wake na uwepo mkubwa kwenye TikTok, hupenda kutozungumzia maisha yake binafsi kwa sabubu “watu wana mambo mengine ya kujali.”[2]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Alianza kuandika muziki akiwa shuleni akizalisha midundo yake mwenyewe. Angepandisha muziki wake kwenye SoundCloud. Mnamo Desemba 2020, aliweka video ya nyimbo yake “Just a Waste” na ikapata umaarufu mkubwa.

Mtindo wa muziki[hariri | hariri chanzo]

Pinkpantheress amesema kuwa waimbaji kama Just Jack, Lilly Allen, My Chemical Romance, Michael Jackson, Lily Allen, Imogen Heap, Haley Williams na Kaytranada ni muhimu kwa mtindo wake  wa muziki.[4] Pia amesema aina za muziki kama Kpop, au muziki wa Pop wa Korea ni muhimu katika mtindo wake. Amesema kuwa kusikiliza aina hizi tofauti za muziki kumemsaidia kukuza mtindo wake wa kipekee.[5]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Tangu kuanza kazi yake kama mwimbaji, ametoa mixtape moja, “To Hell With It” iliyotoka mwaka wa 2021. Baadaye, alitoa albamu yake ya kwanza “Heaven Knows” iliyotolewa Oktoba 13, 2023.

Mbali na miradi hiyo, ametoa nyimbo nyingi kwenye SoundCloud. Pia ametoa nyimbo maarufu kama “Boy’s a Liar Pt.2”, kabla ya kutolewa kwa albamu yake. Mifano mingine ya nyimbo zake maarufu ni “Just For Me”, “Angel” iliyoandikwa kwa kifereji cha sauti cha filamu ya Barbie, “Picture In My Mind”, “Pain”, na nyingine nyingi.

PinkPantheress katika onyesha la kwanza la filamu ya Barbie

Tuzo na mapendekezo[hariri | hariri chanzo]

PinkPantheress amependekezwa kwa tuzo nyingi katika miaka miwili ilyopita. Amechaguliwa kwa tuzo 10. Ameshinda tuzo 2 kati ya hizo: “Best Female Act” kutoka tuzo za MOBO 2022 na BBC Sound ya 2022.[6][7] Amepokea uteuzi wa kuwania tuzo nyingi zaidi lakini hajashinda.

Marejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://theface.com/music/music-pinkpantheress-tiktok-to-hell-with-it-mixtape-pop-drum-and-bass-exactitudes-volume4-issue10
  2. 2.0 2.1 Erica Campbell (2023-02-03). "PinkPantheress: “I don't care about the beats, I care about the pen”". NME (kwa en-GB). Iliwekwa mnamo 2024-04-29. 
  3. Ben Rogersonpublished (2024-02-14). "“I thought it was going to be fine”: PinkPantheress confirms that she lost 80% of the hearing in one of her ears after it was damaged by microphone feedback". MusicRadar (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-29. 
  4. Erica Campbell (2023-02-03). "PinkPantheress: “I don't care about the beats, I care about the pen”". NME (kwa en-GB). Iliwekwa mnamo 2024-04-29. 
  5. PinkPantheress: The 'breakout' singer who's happy to be a mystery (kwa en-GB), 2021-08-25, iliwekwa mnamo 2024-04-29 
  6. PinkPantheress made hits from her bedroom - now she's won the BBC Sound Of 2022 (kwa en-GB), 2022-01-06, iliwekwa mnamo 2024-04-29 
  7. Charlotte Krol (2022-12-01). "MOBO Awards 2022: Little Simz, Knucks, Central Cee, PinkPantheress and Jamal Edwards among winners". NME (kwa en-GB). Iliwekwa mnamo 2024-04-29.