Picha ya kiwamba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Screenshot ya ukurasa huu

Screenshot (pia: kielelezo-skrini) ni picha ya kiwamba au skrini ya kompyuta. Katika Windows ni kazi rahisi kabisa.

Matumizi[hariri | hariri chanzo]

Inasaidia

 • kushika makosa yanayotokea wakati wa kutumia programu za kompyuta
 • Kunakili picha ambazo hazipatikani kwa njia nyingine
 • Mawasiliano na maelewano kati ya watumiaji wa kompyuta wakiwasiliana kwa njia ya barua pepe

Namna ya kufanya picha ya baobonye[hariri | hariri chanzo]

 1. Chagua ukurasa au mwandishi au yale unayotaka kuonyesha na hakikisha yameonekana kwenye kiwamba cha kompyuta yako
 2. halafu fungua programu ya picha - kwa mfano "paint" (ama kupitia Start-All Programs-Accessories-paint AU kupitia start-run - mspaint).
 3. kwenye dirisha unalotaka kuonyesha bofya "print screen" (kwa kawaida juu upande wa kulia kwenye sehemu ya baobonye kwa tarakilishi zingine huandikwa kwa kifupi "prt sc" na kwa vifaa zisizo na baobonye vidunde za kuongezea na kupunguza sauti hutumika[1]). Hutaona badiliko lakini umenakili tayari picha ya skrini yako katika kumbukumbu ya muda.
 4. Katika paint (au programu nyingine ya picha) tekeleza amri ya "paste" (kwa menu edit-paste AU kwa puku right click-paste AU kwa kushika CTRL halafu bofya V).
 5. Amri hii inaingiza picha ya skrini katika dirisha la paint.
 6. Picha hii awali bado si imara, unaweza kuisukuma. Bofya "Esc" halafu ni imara.
 7. Sasa unakata sehemu ile tu ambayo unaitaka kuonyesha halafu unainakili na kuiweka kwa ukurasa mpya ya paint.
 8. Ukurasa huu unahifadhi kama picha ukichagua format ya jpg.
 9. Ukihariri picha unaweza pia kuchora duara nyekundu mahali unapotaka kuonyesha hasa.
 10. Hii faili ya picha unaweza kutuma kwa barua pepe au kuingiza katika wikipedia.

TAHADHARI: Usisahau kubadilisha format kuwa jpg au kile unachotaka kwa sababu pekee yake ni faili kubwa sana ya format ya bmp.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. Raymond, Chen (2014-01-14), "How do I hit the Win+PrintScreen hotkey if my tablet doesn’t have a PrtSc key?", Microsoft | Developer : The Old New Thing (in en-US) (Microsoft), retrieved 2018-09-24 

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]