Nenda kwa yaliyomo

Philo Ikonya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Philo Ikonya ni mwandishi, mwanahabari na mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka Kenya. Makala na vitabu vyake mara nyingi vinazungumzia ya kisiasa nchini Kenya. Alikuwa rais wa tawi la Kenya la chama cha kimataifa cha waandishi[1]. Baada ya kukamatwa mara kadhaa kwa uharakati wake mwaka wa 2009 akiwa chini ya ulinzi wa polisi, aliondoka Kenya kwa kile kilichoitwa uhamisho wa kisiasa.[2]

Maisha ya Kitaaluma[hariri | hariri chanzo]

Mbali na makala za jarida na magazeti, Ikonya amechapisha vitabu vya mashairi na riwaya mbalimbali ikiwemo iliyoitwa kwa jina la Kenya, Will You Marry Me?[3] Pia alitafsiri kitabu cha mashairi cha mshairi wa Kichina Jidi Majia katika lugha ya Kiswahili.[4]

Ikonya alisoma Chuo Kikuu cha Nairobi, ambapo alipata shahada ya uzamili katika fasihi. Amefundisha semiotiki katika Chuo cha Tangaza ambacho ni tawi la Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki.[5]

Uanaharakati[hariri | hariri chanzo]

Akiwa nchini Kenya, Ikonya alikuwa akifanya kazi ya kutetea haki za binadamu na uharakati usio na ukatili na alikamatwa mara mbili tofauti mwaka wa 2007 na 2009.[6] Katika maandamano ya mwaka wa 2008 dhidi ya rais wa wakati huo wa Kenya Mwai Kibaki, alisema, "Kila siku kuna kitu kinatokea ambacho kinaonyesha upande wa viongozi kutojali kwa hivyo kuna kutoridhika ama kukubaliana kwa ujumla."[7]

Mnamo tarehe 18 Februari 2009, Ikonya na wengine wawili walikamatwa nje ya Bunge la Kenya kwenye maandamano dhidi ya mfumuko mkubwa wa bei. Akiwa chini ya ulinzi wa polisi, alipigwa sana na afisa wa polisi wa kiume. Baadaye mwaka huo huo, aliondoka Kenya na kwenda katika Jiji la Makimbilio la Kimataifa huko Oslo, Norway.[8]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Philo Ikonya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.