Philippa Hobbs
Philippa Hobbs (alizaliwa mwaka 1955) ni mwanahistoria na msanii na mkusanyaji wa amali za kihistoria wa Afrika Kusini.
Alimaliza elimu yake kutika shule ya Mtakatifu Andrea mwaka 1972. Alisomea sanaa katika chuo cha sanaa cha Johannesburg kabla ya kumaliza shahada ya uzamili ya uchapishaji katika chuo kikuu cha sanaa Philadelphia. Aliendeleza elimu yake katika chuo kikuu cha Afrika kusini na Technikon Witwatersrand. [1]
Sanaa
[hariri | hariri chanzo]Hobbs alialikwa kuchangia katika picha katika mradi wa haki za binadamu mwaka 1996 uliohusisha wasanii kufanya maonyesho katika katiba ya Afrika ya kusini kifungu cha haki za binadamu. Hobbs' alihusika na kifungu cha 8: Uhuru wa kujieleza ambapo kazi yake ( kinyago) cha ulimi kilionyesha mzani katika kujieleza na matokeo yake. [2]
Kazi nyingine za Other works by Hobbs
Kufundisha
[hariri | hariri chanzo]Hobbs alijifunza pia na kuhudhuria warsha katika studio yake ya uchapishaji ya Foot Pribt studio'.Studio ilianzishwa ili kutoa mafunzo shahir ya uchapishaji kwa wasanii chipukizi na wabobezi.
Machapisho
[hariri | hariri chanzo]Hobbs alichapisha Printmaking in a Transforming South Africa akiwa na Elizabeth Rankin mwaka 1997 (David Philip Publishers), ambacho kilielezea jinsi gani uchapishaji ulivyopitishwa katika idara tofauti kwenye sanaa za nchini Afrika Kusini[3] na aliezezea vigezo vya kitaalamu na kiufundi ndani ya uchapishaji, pia alielezea ni kwa namna gani ilisaidia wakati wa mapambano ya uhuru.
Mwaka 2003 Hobbs na Rankin walichapisha Rorke’s Drift Empowering Prints,[4] ambayo iliangaza juu ya sanaa na uchongaji ndani ya kanisa la Kilutheri, kwa jina maarufu ‘’Rorke's Drift Art and Craft Centre’’. Makala yao inaelezea sanaa iliyotengenezwa na watu weusi waliojifunza katika semina, ikijumuisha mwanafunzi wa kwanza kujiandikisha Allina Ndebele, ambaye, Hobbs amekua akimfanyia utafiti katika machapisho mengine kama ya mwaka 2011 ‘’Water and Space’’, 2014 ‘’Allina Ndebele’s Tree of Life’’, na 2018 ‘’Mantis Wedding: Performing Power in the Loom’’.
Chapisho la Hobbs la mwaka 2006, Messages and Meaning, ni katalogi kwa ajili ya makusanyo ya sanaa ya MTN ambamo ni mtunzaji. Ni mkusanyiko wa insha zilizoandikwa na waandishi tofauti tofauti kama Nessa Leibhammer, Elizabeth Rankin, Wilma Cruise na waandishi nguli wengine. Inachunguza ni kwa namna gani makusanyo hayo ni chombo kwa ajili ya uwekezaji katika jamii, rasilimali kwa ajjili ya elimu, namna na kuhamasisha mawasiliano ya ndani na midahalo, na maonyesho ya sanaa kwa Afrika ya kusini.”[5]
Hobbs amekua na mchango mkubwa pia katika chapisho la sanaa ya Afrika kusini maarufu kwa jina la, Taxi. Pamoja na ushiki huu, amekua akiandika sambamba na ‘’TAXI Art Education Supplement’’ kwa ajili ya wanafunzi- akiruhusu taarifa zipatikane kwa urahisi.[6]
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]- 1975 Fine Art Award, Johannesburg College of Art
- 1978 Orodha ya mshauri (Philadelphia College of Art, USA)
- 1987 Rector's Medal, Technikon Witwatersrand (kwa masomo ya astashahada ya juu)
- 1987 Finalist and Merit Award winner, Volkskas Atelier Awards, Pretoria
- 1987 Chamber of Mines Award, TWR (For Higher Diploma studies)
- 1988 Finalist, AA Vita Awards, Johannesburg
- 1988 Finalist, Cape Town Triennale, Cape Town
- 1994 Alumnus Award, Technikon Witwatersrand
- 2004 Business Arts South Africa Award (Special Project) for exhibition and publication Rorke’s Drift: Empowering Prints
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ http://www.durbanet.co.za/exhib/dag/hr/cl08.htm
- ↑ http://www.durbanet.co.za/exhib/dag/hr/cl08.htm
- ↑ Hobbs, P., Rankin, E. 1997. Printmaking in a Transforming South Africa. Claremont: David Philip Publishers.ISBN 0-86486334-9
- ↑ Hobbs, P., Rankin, E., 2003. Rorke’s Drift Empowering Prints. Cape Town: Double Story Books.ISBN 1-919930-13-2
- ↑ Hobbs, P. (ed.) 2006. Messages and Meaning. Johannesburg: David Krut Publishing.ISBN 0-9584860-6-9
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2021-04-10.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Philippa Hobbs kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |