Nenda kwa yaliyomo

Patapotea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Patapotea
Jalada la Patapotea
MwandishiJaphet Nyang'oro Sudi
NchiTanzania
LughaKiswahili
AinaUpelelezi
Set inKigoma, Arusha
Kimechapishwa2018
MchapishajiPapaso Publishers
Tarehe ya kuchapishwa
2018
Aina ya MediaKaratasi
Kurasa300+
ISBN978-9987-794-08-9

Patapotea ni riwaya ya kipelelezi iliyoandikwa na Japhet Nyang'oro Sudi inayozungumzia mkasa wa muandishi wa kitabu cha Saa 72 anaejiingiza matatizoni baada ya kuwa ametoka mkoani Arusha kwenda Kigoma kumfuatilia Mwendawazimu mmoja aliejitolea kufa wakati akiokoa kitabu kisiungue ndani ya kijumba chake kilichokuwa kinaungua moto.[1]

Mwendawazimu huyo alifanya tukio la kuingia ndani ya nyumba inayowaka moto baada ya kuichomwa moto na watu wa manispaa ua mji wa Kigoma.

Tukio hilo lina washangaza wengi na ndipo mtunzi wa kitabu hicho anapoamua kufunga safari ya kutoka Arusha kwenda kumtafuta mwenda wazimu huyo bila ya kufahamu matatizo anayokwenda kukumbana nayo huko mbele na baadae kujikuta akiangukia nchini Congo katika mikono ya waasi. [2]

  1. Sudi, Japhet Nyang'oro, 1981-. Patapotea. Dar es Salaam. ISBN 978-9987-794-08-9. OCLC 1089276051.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)
  2. "PATAPOTEA Page". www.somariwaya.co.tz. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-05-08. Iliwekwa mnamo 2020-02-07.