Omo
Mandhari
Omo ni sehemu ya mbele ya meli, merikebu, dau au chombo kingine cha bahari. Sehemu ya nyuma huitwa tezi au shetri.
Omo inatakiwa kuwa nyembamba kwa sababu ni sehemu inayokata mawimbi. Kama ni pana mno linasukuma maji mengi na kuchelewesha mwendo wa chombo. Vivuko (feri) na meli za kijeshi za kushushia magari au askari ufukoni zina omo pana.
Kwa meli au jahazi zenye mbio omo linahitaji kuwa kubwa kwa kutosha ili maji yasimwagwe juu ya chombo wakati wa mwendo.
-
Omo la meli ya kontena.
-
Sanamu omoni la jahazi kubwa "La Recouvrance".
-
Omo la jahazi la "Cutty Sark"
-
Omo la meli ya kushushia magari ya kijeshi na askari ufukoni