Nenda kwa yaliyomo

Oliver Queen (Smallville)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Oliver Queen
Faili:OQueenFinale.jpg
Imechezwa na Justin Hartley
Maelezo
Familia Chloe Sullivan (mke), Robert Queen na Laura Queen (wazazi, wamefariki)

Oliver Jonas Queen [1] ni jina la mmiliki bilionea na ni CEO wa Queen Industries, ambaye pia anajulikana kwa jina la Green Arrow. Huyu pia ni mume wa Chloe Sullivan. Akiwa kama Green Arrow, Oliver anavaa vazi la kijani na nyeusi na kuamuru aina mbalimbali za mishare na zana kwa ajili ya ulinzi.

Oliver amepata kuwa na mahusiano marefu kiasi na Lex Luthor. Uhusiano ambao ulianza wakati wanasoma wote katika shule ya bweni. Pia amewahi kuwa na mahusiano ya kimahaba-kiutatanishi na mfuasi wa Lex Luthor, Tess Mercer. Yeye ndiye mwanzilishi wa kikosi cha mashujaa-bab-kubwa, ambamo ni kikosi cha watu kilichojianzisha kwa ajili ya kuilinda Metropolis.

Pale Oliver alivyoingiwa na huzuini baada ya kugundua ya kwamba Lionel ndiye aliyewauwa wazazi wake, akabadili maisha yake kwa kuwa mtu wa wanawake, ulevi, na kujirusha. Haitoshi tena ameacha hadi kazi zake za Green Arrow na kutumia miezi mingi kwa kutengeneza kurasa za umbeya kufuatia kifo cha Jimmy Olsen, lakini baadaye akaamua kurudi katika hali ya kawaida kama jinsi alivyokuwa hapo awali (ilikuwa kwa msaada wa Chloe Sullivan.

Uhusiano wake

[hariri | hariri chanzo]

Uhusiano wa Kirafiki na Wanaume

Uhusiano wa Kirafiki na Wanawake

  • Chloe na Oliver: Inaelezea jinsi walivyokutana na kuhusiana kikazi na hadi hapo baadaye kimapenzi.
  • Lois na Oliver: Inaelezea uhusiano wao mfupi wa kimahaba na urafiki wa kufa na kuzikana.
  • Tess na Oliver: Inaelezea utatanishi wa urafiki wao.
  • Clark, Lois na Oliver: Inaelezea mapenzi-kizungu-mkuti waliogawana na urafiki wao wa kina.
  1. Oliver's middle name is spoken by his father in Volume 1 of the Oliver Queen Chronicles

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]