Nikola Kalinić
Nikola Kalinić (alizaliwa 5 Januari 1988) ni mchezaji wa klabu ya Kroatia ambaye anacheza kama mshambuliaji wa klabu ya Hispania iitwayo Atlético Madrid na timu ya taifa ya Kroatia. Kalinić alianza kazi yake na klabu ya Hajduk Split iiliyopo nchini kroatia kabla ya kuhamia Uingereza katika klabu ya Blackburn Rovers kwa £ 6,000,000 mwaka 2009.
Kazi ya klabu
[hariri | hariri chanzo]A.C. Milan
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 22 Agosti 2017, Kalinić alijiunga na klabu ya A.C. Milan kwa mkopo na baadaye kununuliwa kwa ada ya € 25,000,000. Alichagua kuvaa jezi nambari 7.Aliweza kushinda katika mechi ambayo walishinda 2-1 dhidi ya Cagliari mnamo Agosti 27, akiingia kama mbadala katika dakika ya 78.
Atletico Madrid
[hariri | hariri chanzo]Tarehe 9 Agosti 2018, Atlético Madrid ilimsaini Kalinić kwenye mkataba wa miaka mitatu(3).Alicheza La Liga kwa mara ya kwanza mnamo 1 Septemba, na kupoteza 0-2 dhidi ya Celta Vigo akiingia kama mbadala katika dakika ya 56. Mnamo tarehe 8 Desemba 2018, alianza katika mchezo dhidi ya Alaves badala ya Diego Costa aliyejeruhiwa na kufunga bao lake la kwanza katika ushindi wa magoli 3-0 nyumbani.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nikola Kalinić kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |