Jeshi la majini
Mandhari
(Elekezwa kutoka Nevi)
Jeshi la majini au Jeshi la wanamaji ni kitengo cha pekee cha jeshi la mataifa mengi kilicho tayari kushindana na maadui kwenye maji hasa baharini.
Linajumlisha askari, manowari, meli za kusaidia manowari, bandari ya pekee na vituo vingine na pia eropleni za vita ya bahari.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Ni hasa nchi zenye pwani ya bahari ambako kuna jeshi la pekee la wanamaji. Chanzo katika historia yalikuwa majeshi ya wanamaji ya Karthago, Ugiriki ya Kale na Dola la Roma.
Tangu karne ya 19 Uingereza ilikuwa na jeshi la wanamaji kubwa duniani, na katika karne ya 20 nafasi yake ilichukuliwa na wanamaji wa Marekani hasa, lakini pia wa Urusi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |