Nevado Mismi
Mandhari
Nevado Mismi ni mlima katika Andes za Peru.
Ina kimo cha 5,597 m juu ya UB kipo 20 km upande wa kaskazini kutoka mji wa Chivay katika mkoa wa Arequipa takriban 160 km upande wa magharibi wa ziwa Titicaca na 700 km upande wa kaskazini kutoka Lima mji mkuu wa Peru. Mlima una barafuto kadhaa juu yake.
Tangu 2001 Nevado Mismi imetangazwa kuwa chanzo cha mto Amazonas. Barafuto za Nevado Mismi ni chanzo cha mto Río Apurímac unaopeleka maji yake kupitia mito ya Río Ene, Río Tambo na Río Ucayali kwenda kaskazini hadi kufikia mto Marañón unaoingia katika mwendo wa Amazonas.
Kwa ujuzi wa kisasa chanzo cha Río Apurímac ni chanzo cha mbali kutoka mdomo wa Amazonas.