Netarsudil
Netarsudil, inayouzwa kwa jina la chapa Rhopressa na Rhokiinsa, ni dawa inayotumika kutibu shinikizo la ndani ya jicho lililoongezeka ikiwa ni pamoja na glakoma ya pembe-wazi (open-angle glaucoma).[1][2] Dawa hii inatumika kama tone la jicho.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na macho mekundu, kutokwa na damu kwenye utando wa jicho, uoni hafifu na kuchanika.[2] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha uvimbe wa konea unaosababishwa na bakteria (keratiti ya bakteria).[2] Dawa hii ni kizuizi cha enzimu ya rho kinase (inayodhibiti sura na harakati za seli).[2]
Netarsudil iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2017, na Ulaya mwaka wa 2019.[2][1] Nchini Marekani, chupa ya mililita 2.5 inagharimu takriban dola 305 za Marekani kufikia mwaka wa 2021.[3] Dawa hii inapatikana pia kama mchanganyiko wa netarsudil/latanoprost.[2] Haijakuwa ikipatikana kibiashara katika Ulaya na Uingereza kufikia mwaka wa 2021.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 "Rhokiinsa EPAR". European Medicines Agency (EMA). 16 Septemba 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Desemba 2019. Iliwekwa mnamo 27 Septemba 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 "Netarsudil Mesylate Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Juni 2020. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Rhopressa Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Netarsudil". SPS - Specialist Pharmacy Service. 25 Januari 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Novemba 2021. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Netarsudil kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |