Nenda kwa yaliyomo

Nepafenaki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nepafenaki (Nepafenac), inayouzwa kwa jina la chapa Nevanac miongoni mwa mengine, ni dawa ambayo hutumiwa kupunguza maumivu, kuleta chini joto la juu na mwasho unaohusishwa na upasuaji wa lenzi ya jicho.[1] Dawa hii inatumika kama tone la jicho.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuwasha kwa jicho.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha keratiti na hyphema.[2] Inafanya kazi kwa kuzuia COX-1 na COX-2 na kwa hivyo kupunguza vitu vinavyofanana na homoni vinavyoathiri kazi kadhaa za mwili, ikiwa ni pamoja na mwasho, maumivu na mikazo ya uterasi (prostaglandini).[2][1]

Nepafenaki iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2005 na Ulaya mwaka wa 2007.[2][1] Nchini Uingereza, chupa moja hugharimu Huduma za Afya za Kitaifa (NHS) takriban £15 kufikia mwaka wa 2021.[3] Nchini Marekani, kiasi hiki kinagharimu takriban dola 290 za Marekani.[4]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Nevanac". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Julai 2020. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 "Nepafenac Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Aprili 2016. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1206. ISBN 978-0857114105.
  4. "Nevanac Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Mei 2020. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nepafenaki kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.