Natalia da Rocha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Natalia da Rocha
Amezaliwa Natalia da Rocha
Afrika Kusini
Jina lingine Natalia
Kazi yake Mwigizaji na Mwongozaji


Natalia da Rocha akiwapongeza watazamaji kwa kuhudhuria onyesho la hadithi yake
Natalia da Rocha akiwapongeza watazamaji kwa kuhudhuria onyesho la hadithi yake.

Natalia Da Rocha ni mwigizaji, mwongozaji, mhamasishaji wa vijana na mfanyabiashara wa Afrika Kusini. Atakumbukwa kwa kuwa miongoni mwa watu wachache weusi walioonekana katika vyombo vya vitumbuizo wakati wa ubaguzi wa rangi. Mwaka 1981, alikuwa mtu wa kwanza mweusi kuhitimu shahada ya uigizaji katika chuo kikuu cha Stellenbosch. Mwanzoni mwa mwaka 1987, alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi akiwa pamoja na Sam Marais kuwa nyota katika tamasha la Suncity. Mwaka 1992 alikuwa nyota wa kwanza kutoka Afrika ya Kusini kufanya maonyesho ya wazi nchini Madagascar. Anakumbukwa vema kwa kazi yake katika muziki kama vile Ain't Misbehavin, Midnight Blues, Godspell na Vere.

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Natalia da Rocha kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.