Mtumiaji:Salum Kim Mwandishi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

SALUM KIM MILONGO ni Mwandishi wa Vitabu, Mtanzania wa kuzaliwa 02 Disemba Iringa, msomi wa shahada ya Ualimu. Salum ni mlumbi wa lugha ya Kiswahili pia ni msimuliaji wa kazi za fasihi ya Kiswahili na mwandishi wa vitabu vya historia za watu maarufu nchini.

Ameandika vitabu vingi kikiwemo kitabu cha William Malecela chenye kichwa “My American Experience” pia ameandika vitabu vingi vya hadithi za watoto na vitabu vya historia za koo mbalimbali. Orodha ya vitabu alivyoandika ni pamoja na;

  1. "Mtoto wa Nuru" cha Mc Pilipili
  2. "Baba wa Sanaa" cha Rugemarila Mutahaba
  3. “My American Experience” cha William Malecela
  4. Uongozi na Maisha cha Richard Kasesela
  5. Taarifa ya kazi za Mbunge (2015- 2020) Subira Khamis Mgalu "Ripoti"
  6. Taarifa ya kuhusu huduma kwa Mtoto (Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam) Paul C. Makonda
  7. Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015 -2020 Jimbo la Amani Zanzibar. Mussa H. Mussa
  8. Ukombozi wa Fikra cha Winfrida Shonde
  9. Ujana na Uongozi cha Kenan Leban Kihongosi
  10. Mimi Maya "Historia ya Maisha ya Mayness Chapote"


Kim ni muendeshaji wa programu inayoendeshwa katika mitandao ya kijamii iitwayo “HATUTO KUACHA” programu iliyojikita katika maswala ya kijamii kwa kuchambua muktadha wa mambo ya dini na imani. Sambamba na hayo Kim kwa kushirikiana na Grids Solution Tanzania, wameendelea kuongoza katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile;

  1. Kufanya utafiti
  2. Kuandika, kuhariri, kupanga na kuchapa vitabu.
  3. Ushauri wa masoko
  4. Usambazaji wa vitabu.