Mtumiaji:SHERIA KWA KISWAHILI

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sheria kwa Kiswahili kwa kiingereza "law in Kiswahili" ilianzishwa mwaka 2013 mwanzilishi wake akiwa ni Ofmedy Mtenga ambaye kwa taaluma ni Mwanasheria. Lengo kuu la maudhui haya ni kutafsiri sheria kutoka kiingereza kwenda kiswahili kwaajili ya wasomaji wa sheria wasiojua kiingereza. walengwa wakubwa wa tafsiri za sheria kwa kiswahili ni wananchi wa kawaida ambao sio wanasheria ila wanapenda kupata mwanga juu ya sheria za Tanzania.

kwa muktadha huo Ofmedy Mtenga ameshaandika vitabu kadhaa vya sheria kwa kiswahili vikiwemo vile vinavyohusu Sheria ya Ndoa Tanzania, Sheria ya Mirathi na Wosia, Haki ya Kupata dhamana polisi na mahakamani na haki za watoto waliozaliwa nje ya ndoa. vitabu vyote hivi vinapatikana katika ukurasa wake wa blog iitwayo www.sheriakwakiswahili.blogspot.com' eneo ambalo watu wanaweza kupata aina mbalimbali za sheria za Tanzania bure kwa kupakua toka kwenye mtandao.

kwa wenyeji wa Tanzania, vitabu hivi vinapatikana maduka yaliyoko mikoa yote Tanzania vilevile, ukiingia kwenye blog yake utakutana na namba za simu zitakazokuelekeza wapi vitabu vinapatikana kwa wanaohitaji.