Mtumiaji:Rev.Prof. Ketaro/ukurasa wa majaribio
Maana Ya Mtu
Neno la Kiswahili "Mtu" etimolojia yake ni kutoka katika maneno ya lugha za Kibantu "Omonto/Mndu/Mnu" ambapo katika lahaja za Kikurya na Kisimbiti lilitoka neno "Omonto" ambalo lilimaanisha "Aliye wa Nto" ambapo neno hilo la Kibantu "Omo" huwakilisha neno la Kiswahili "Aliye wa" na ambapo halikadhalika neno hilo la Kibantu "Nto" huwakilisha neno la Kiswahili "Mtu".[1]
Hivyo basi, kiujumla neno la Kibantu "Omonto" humaanisha "Mtu wa Nto" ambapo kwa lugha ya Kiswahili neno hilo hutamkwa "Mtu". Kitamaduni kuna aina nne za makundi ya Watu ambapo mtu wa daraja la kwanza huaminiwa kuwa "Mungu" ambaye kujitambulisha kwa sifa za kipekee zilizo tofauti na sifa za makundi mengine ya watu ambapo sifa hizo ambazo humtofautisha na watu wengine wote huwa ni pamoja na yeye kuwa asili ya vitu vyote,hana mwanzo wala mwisho wa kuwapo kwake,yupo mahali pote kwa wakati mmoja na wakati wote na kuwa asiyetokana na asili ya kuumbwa.
Aina ya pili ya watu ni wale watu walio wa daraja la pili kimamlaka ambao kiutamaduni hutambuliwa kama wenye sura na mfano wa Mungu, watu ambao mfumo wao wa fahamu za nasfi hujengwa na jumla ya mihimili 6 ya kinafsi ambayo hujumuisha fikra huru,akili, dhamiri,fikra kikomo,utashi na silika ambapo kiutamaduni kundi hili la watu hutambuliwa kama Watu wenye fikakidha (Fikra huru,akili na dhamiri).
Aina ya tatu ya watu ni wale wasio na miili yenye asili ya ardhi ambapo kundi hili hujumuisha nafsi au roho wakiwemo malaika wa aina zote wema kwa wabaya. Watu hawa wa jamii ya malaika pia mfumo wao wa kinafsi umejengwa na jumla ya mihimili 6 ya fahamu za kinafsi sawa na walivyo watu wa daraja la pili kimamlaka.
Aina ya nne ya Watu ni wale watu ambao mfumo wao wa fahamu za kinafsi hujengwa na jumla ya mihimili 3 ya nafsi ambayo hujumuisha fikra kikomo,silika na utashi wao pekee.
Hivyo basi, kiutamaduni neno "Mtu" humaanisha "Nafsi au Roho/roho" iliyo hai.
- ↑ 1. Saikolojia Na Anthropolojia Ya Kiutamaduni Ya Watu Na Wanadamu Wa Kale Na Sasa (ISBN:9789912407770). 2.The Holy Bible In Kiswahili Union Version