Mtumiaji:Mnanka12

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Utakatishaji wa fedha haramu[hariri | hariri chanzo]

Utakatishaji wa fedha ni kitendo cha kuficha asili ya fedha ambazo zinatokana na uhalifu. Mtu anayekatakata fedha anajaribu kuficha kwamba fedha hizo zimepatikana kwa njia mbaya, kwa kuziweka kwenye mfumo wa kifedha halali.

Aina mbalimbali za uhalifu zinazopelekea kutakatisha fedha[hariri | hariri chanzo]

Fedha haramu zinazoweza kutakatishwa zinaweza kutokana na aina mbalimbali za uhalifu kama vile:-

  • Uhalifu wa madawa ya kulevya, biashara ya dawa za kulevya huzalisha kiasi kikubwa cha fedha haramu. Wauzaji wa dawa za kulevya hutumia mbinu mbalimbali kutakatisha fedha zao, kama vile kununua mali, kuwekeza katika biashara halali, au kuhamisha fedha kupitia akaunti za benki za kigeni.
  • Uhujumu uchumi, uhujumu uchumi ni kitendo cha kudhuru uchumi wa nchi kwa makusudi. Kwa mfano ufisadi, wizi wa mali ya umma, na ulaghai wa kodi. Wahalifu wanaohusika na uhujumu uchumi mara nyingi hutumia utakatishaji wa fedha kuficha faida zao haramu.
  • Ugaidi, vikundi vya kigaidi hutumia utakatishaji wa fedha kufadhili shughuli zao. Wanaweza kutumia mbinu mbalimbali kutakatisha fedha zao, kama vile kutumia mashirika ya misaada ya uwongo, kuhamisha fedha kupitia akaunti za benki za kigeni, au kutumia biashara halali kama vile maduka ya vyakula au migahawa.
  • Biashara haramu, biashara haramu, kama vile biashara ya binadamu, biashara ya viungo haramu, na biashara haramu ya wanyamapori, huzalisha kiasi kikubwa cha fedha haramu. Wafanyabiashara haramu mara nyingi hutumia utakatishaji wa fedha kuficha faida zao haramu.

Madhara ya utakatishaji fedha[hariri | hariri chanzo]

  • Kudhoofisha uchumi, utakatishaji wa fedha huingiza fedha haramu katika mfumo wa kifedha halali, jambo ambalo linaweza kusababisha mfumuko wa bei pamoja na kusababisha kuporomoka kwa uchumi.
  • Kuharibu sifa ya nchi, nchi zinazoonekana kuwa na viwango vya juu vya utakatishaji wa fedha zinaweza kupata sifa mbaya, jambo ambalo linaweza kuathiri vibaya biashara na utalii.
  • Kuendeleza Uhalifu, Fedha zilizotakatishwa mara nyingi zinatokana na shughuli haramu kama vile ulanguzi wa dawa za kulevya, biashara ya silaha, au ufisadi. Utakatishaji fedha huwezesha uhalifu kuendelea kwa kuficha asili yake na kuzirudisha fedha hizo kwenye uchumi halali.

Hitimisho[hariri | hariri chanzo]

Utakasishaji wa fedha ni tatizo kubwa la kimataifa lenye madhara makubwa kwa jamii. Serikali na taasisi za kimataifa zinachukua hatua mbalimbali kupambana na utakatishaji wa fedha. Hatua hizi ni pamoja na kuanzisha sheria na kanuni za kupambana na utakatishaji wa fedha Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu, pamoja na kuongeza ufahamu kwa umma kuhusu utakatishaji wa fedha.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

[1] [2]

  1. https://www.fiu.go.tz/FedhaHaramuNiNini.asp
  2. https://www.judiciary.go.tz/web/index.php?r=posts%2Fwebview&id=790