Mtumiaji:Mlapa Ng'osha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Gabriel Samalu Ng’osha, ni kijana mwanaharakati, mjasiriamali, msanii wa muziki, mtunzi, mwimbaji, muigizaji na mwandishi kutoka nchini Tanzania(amezaliwa 1985) anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Mlapa Ng’osha. Alianza rasmi muziki mwaka 1999, mwaka 2013 alifanikiwa kurekodi wimbo wa kwanza akiwa na rafiki yake Lameck aka Buchanagandi, mwaka 2005 alirekodi wimbo wa ‘kifo’ chini ya produzya Kid Bway wa Tetemesha rekodi, mwaka 2007, wimbo wa ‘Njaa’ akiwa na rafiki yake Chid Mago wakiunda kundi la Pond Mobb. === Mwaka 2012 alifanya wimbo wa ‘Mauaji haya’ akishirikiana na Kala Jeremiah (Mshindi wa tuzo tatu mwaka 2013, tuzo ya Msanii bora wa hip hop , mtunzi bora wa mashairi ya hip hop, na wimbo bora wa mwaka) ambaye pia ni zao la BSS (Bongo Star Search) mwaka 2009, wimbo wa ‘Huruma’ akimshirikisha mshindi wa EBSS (Epiq Bongo Star Search), mwaka 2013 , Emmanuel Msuya, kwa sasa anatamba na wimbo wake wa ‘Kalale pema’(Mjamzito) wimbo unaozungumzia matatizo wanayoyapata wakina mama wajawazito katika nchi zinazoendela kabla na baada ya kujifungua.

Ni mwanzilishi na mwasisi wa Kikundi Amkeni Vijana (KIAVI, kilianzishwa mwaka 2010, Mkoani Mwanza) ambacho kwa sasa inajulikana kama taasisi ya Maisha Pa1 inayoshughulika na masuala ya mama wajawazito pamoja na Vijana.

Taasisi hiyo kwa sasa inafanya mradi wa kuhamasisha jamii ya Watanzania kuhakikisha inapunguza ama kutokomeza kabisa vifo vya kina mama wajawazito kabla na baada ya kujifungua, kupitia kauli mbiu ya ‘MAISHA PA1 OKOA WAJAWAZITO’. Mawasiliano:maishapa1@gmail.com au Maisha Pa1.blogspot.com