Mtumiaji:Magotech/Mhemko hasi
Mhemko hasi katika saikolojia ya mbinu za kujilinda na kujidhibiti, ni kitendo kinachochukuliwa kuwa kibaya au kisicho cha kijamii.[1] Kwa ujumla kitendo hiki huchukuliwa kuwa ni cha uharibifu kwa mtu binafsi na kwa wanaomzunguka. Neno hili hutumiwa kwa njia hii katika uraibu wa ngono, matibabu ya kisaikolijia, uhalifu na malezi. Kinyume chake huchukuliwa kama mtazamo au tabia tofauti ya kuweza kujidhibiti na msukumo hasi, kitendo hicho hujulikana kama mhemko chanya.
Kitendo kinachofanywa kufuata msukumo wa uraibu (mfano:ulevi,utumiaji wa madawa ya kulevya au wizi).Pia inaweza ikawa njia iliyotengenezwa(mara nyingi bila ufahamu au ufahamu mdogo) ili kujionyesha (mfano kuonyesha hasira kali au kufanya uasherati). Mhemko hasi unaweza kuzuia maendeleo /ukuaji wa muitikio wenye kujenga zaidi kwa hisia husika (hisia zinazo mkabili mtu zisizo na majibu).
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Kasik, Maribeth Montgomery (2008-07-15), Reynolds, Cecil R.; Fletcher-Janzen, Elaine (whr.), "Acting Out", Encyclopedia of Special Education (kwa Kiingereza), John Wiley & Sons, Inc., ku. speced0039, doi:10.1002/9780470373699.speced0039, ISBN 978-0-470-37369-9, iliwekwa mnamo 2022-11-26