Mtumiaji:Madaula
Wikipedia:Babel | |||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mimi ni mshiriki wa Google Health Speaks. Jina langu ni Dr Marina Alois Njelekela. Mimi ni Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kishiriki cha Sayansi za Afya Muhimbili Dar es Salaam Tanzania. Nilizaliwa hapa Dar es salaam tarehe 23 mwezi julai mwaka elfu moja mia tisa sitini na nne. Ni mtoto wa tatatu katika familia ya watoto saba. Elimu yangu ya msingi nilipata katika mikoa mbali mabli ikiwemo Mtwara, Ruvuma, Mara na kumalizia Dar es Salaam katika shule ya msingi Forodhani kwa sasa Shule ya Mtakatifu Josemph ya Millenium. Elimu ya sekondarinilipatia katika shule za sekondari Zanaki na Ndanda huko Mtwara. Nilijiunga na Chuo Kikuu Cha Afya cha Muhimbili mnamo mwaka 1987 na kufanikiwa kupata shahada ya kwanza ya udaktari mnamo mwaka 1993. Mafunzo ya awali yakazi ya udaktari (internship) nilipatia Hospitali ya KCMC Moshi. Nilianza kazi rasmi ya Udaktari mwaka 1995 katika hospitali ya Agakhan, baada ya hapo nilifanya kazi kitengo cha mifupa Muhimbili kabla ya kuajiriwa kama Mhadhiri Msaidizi katika chuo kikuu cha Muhimbili mwaka 2001.Nimeendelea kufundisha hapo chuoni mpaka sasa katika Idara ya Fisiolojia ambapo kwa sasa ni Mkuu wa Idara hiyo. Mimi pia ni mtafiti wa masuala ya magonjwa sugu kama saratani, kisukari, shinikizo la damu na unene kupita kiasi. Na pia natafiti mahusiano ya magonjwa hayo na tabia zetu hasa katika vyakula, mazoezi ya mwili, uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe nk.