Vifuko Vidogo vya Seli

Vifuko Vidogo vya Seli (huitwa VVS kwa ufupi au extracellular vesicles kwa Kiingereza) ni viputo vidogo vilivyofunikwa na utando wa mafuta (lipidi). Vinatolewa na seli ya asili ambayo inaweza kuwa ya aina ya prokaryoti au yukaryoti. VVS havina vifaa vyote vya kuendeleza uhai, kama mfumo wa kujitengeneza tena, kama vile mitochondria, hivyo haviwezi kuishi kama seli kamili. Vina ukubwa tofautitofauti, na vinabeba vitu mbalimbali vya mwili kama protini, ishara ya protini, fati/lipidi, vinasaba, mfumo wa kutengenezea RNA, mfumo wa kutengenezea vinasaba, mfumo wa kutengenezea protini, kimeng'enya, na vitu vingi vingine kutoka kwenye seli asili (au seli chanzo) kwenda kwenye seli nyingine. Kila kitu kilichoko katika VVS kinatokana na seli iliyokitoa.[1]
Seli chanzo inazalisha VVS kila wakati, iwe katika mwili wa mtu mwenye afya au mgonjwa. VVS hubeba taarifa kutoka seli chanzo na kusaidia katika mawasiliano ya seli hadi seli. seli inapopokea VVS inaweza kubadilika kitabia kulingana na tabia ya vesikeli hiyo.[1]
VVS na Sayansi
[hariri | hariri chanzo]
Katika sayansi, kuna shirika la kimataifa linaloitwa "International Society for Extracellular Vesicles ambalo linafanya utafiti kuhusu VVS.[2] Kuna jarida la VVS pia linaloitwa "Journal of Extracellular Vesicles."[3]
Wanasayansi ambao wanafanya utafiti katika VVS wanatafuta uwezekano wa VVS kuwa kifaa cha kuchunguza mwili na kubainisha magonjwa kama kansa, mvilio wa damu moyoni, na maradhi ya bakteria au kimelea[1][4][5]. Wakati wa ugonjwa seli za mwili zinaongeza VVS maalumu, kama vinasaba maalumu ambavyo wanasayansi wanaweza kuchukua, kuchunguza, na kubainisha mfumo wa ugonjwa. VVS ziko katika majimaji ya mwili kama damu, mkojo, maziwa, majimaji katika ubongo na uti wa mgongo, na mate. Ndiyo sababu kuna urahisi wa kuchukua VVS vinatoka mwilini. Kama daktari au wataalamu wa afya wakiweza kutumia VVS kupata taarifa za mgonjwa, wanaweza kutumia VVS kutambua ugonjwa katika hatua za awali.[1][5]

Katika uzee, VVS vinasaidia mawasiliano kati ya seli katika sehemu mbalimbali za mwili. VVS hizi ni muhimu katika maendeleo ya uzee na maendeleo ya magonjwa yanayohusiana na uzee. Zinajihusisha na mawasiliano ya aina ya endokrini na parakrini. VVS za uzee hujulikana kama SASP (senescence-associated secretory phenotype). Wanasayansi wanafanya utafiti kuhusu matumizi ya VVS kwa wazee na magonjwa ya uzeeni.[6]
Aina ya VVS
[hariri | hariri chanzo]Kwenye mwili, mimea, bakteria, na vitu vingine vya uhai, kuna aina tofauti za VVS. Aina dogo ni supamiru (supermere kwa kiingereza). Tunaelewea supamiru dogo kuliko aina zingine ya VVS. Ina udogo wa 35nm, ni dogo kuliko aina zote za VVS.[1]
Aina kubwa ni onkosomu (oncosome kwa kiingereza). seli za sarakani na zenye tabia ya amiba hutoza onkosomu. Onkosomu ni kama mwili wa apoptiki, lakini ni tofauti kwa sababu ya tabia za seli: onkosomu hutoka seli za sarakani lakini mwili wa apoptiki hutoka seli za afia nzuri. Onkosomu ina ukubwa wa 1000-10000nm, ni kubwa kuliko aina zote za VVS.[1]
Eksosomu (exosome kwa kiingereza) inatoka katika mifuko ya ndani ya seli iitwavyo endosomu (endosome kwa kiingereza). Endosomu zitakapokuwa bado endosomu zitakuwa MVB (mwili unaobeba vifuko vidogo, multivesicular bodies kwa kiingereza). Ukuta wa MVB ukiungana na ukuta wa seli, utatoza rasimali ya MVB. Rasimali hii ni eksosomu (endosomu, lakini ni nje ya seli). Eksosomu ina ukubwa wa 50-150nm.[1]
Maikrovesekali (microvesical kwa kiingereza) ni kama eksosomu, lakini ni yenye ukuta wa mafuta ya seli. Kalisi na mifupa ya seli zitasababisha uvimbe kwenye ukuta wa seli. Ndani ya uvimbe kuna rasimali ya seli. Uvimbe ikijiachia seli inakuwa maikrovesekali. Maikrovesekali ina ukubwa wa 100-1000nm.[1]
Mwili apoptiki (apoptik bodies kwa kiingereza) ni matokeo ya seli inayokufa. Apoptoses ni njia kuu ya kupunguzia seli ya mwili. seli hufanya apoptoses huleta mwili apoptiki ambayo ni sehemu ya seli hadi itakapokufa. Mwili apoptiki ina ukubwa wa 100-5000nm.[1]
Exomiru (exomere kwa kiingereza) ni matokeo ya kukata uvimbe ukubwa kutoka ukuta wa seli. Ni kama maikrovesekali lakini ni bila kalisi na mifupa ya seli. Exomiru inaweza kuwa na ukubwa hadi wa 50nm.[1]
Migrasomu (migrasome kwa kiingereza) zinatoka katika mfumo wa mwili wa seli ambayo inajisogeza. Njia inayojisogeza seli ya mwili inaitwa uhamaji wa seli. Wakati upande mmoja wa seli ikisogea na upande mwingine unasimama, upande huo ambao unasogea utatumia mifupa ya seli kuachia na utatoa migrasomu. Migrasomu ina ukubwa wa 500-3000nm.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 Kumar, M.A., Baba, S.K., Sadida, H.Q. et al. “Extracellular vesicles as tools and targets in therapy for diseases.” Signal Transduction and Targeted Therapy 9, 27 (2024), https://doi.org/10.1038/s41392-024-01735-1.
- ↑ International Society for Extracellular Vesicles. “About the International Society for Extracellular Vesicles.” International Society for Extracellular Vesicles (ISEV), 2021, https://www.isev.org/about-isev.
- ↑ International Society for Extracellular Vesicles. “Journal of Extracellular Vesicles.” International Society for Extracellular Vesicles (ISEV), 2021, https://www.isev.org/JEV.
- ↑ A. Phillip Owens and Nigel Mackman and Christian Weber and Sebastian Mause. “Microparticles in Hemostasis and Thrombosis.” Circulation Research, Volume 108, Number 10, Pages 1284-1297, 2011, DOI 10.1161/CIRCRESAHA.110.233056, https://www.ahajournals.org/doi/abs/10.1161/CIRCRESAHA.110.233056.
- 1 2 Seiji Yamamoto, Erika Azuma, Masashi Muramatsu, Takeru Hamashima, Yoko Ishii, Masakiyo Sasahara. “Significance of Extracellular Vesicles: Pathobiological Roles in Disease, Cell Structure and Function.” J-STAGE, Volume 41, Issue 2, Pages 137-143, 2016, Online ISSN 1347-3700, Print ISSN 0386-7196, https://doi.org/10.1247/csf.16014 https://www.jstage.jst.go.jp/article/csf/41/2/41_16014/_article/-char/en.
- ↑ Oh C, Koh D, Jeon HB, Kim KM. “The Role of Extracellular Vesicles in Senescence”. Molecules and Cells, 30 September 2022, 45(9):603-609. doi: 10.14348/molcells.2022.0056. Epub 2022 Aug 31. PMID: 36058888; PMCID: PMC9448646.