Mtumiaji:Joseph Mlay

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

MAKALA YA KWANZA[hariri | hariri chanzo]

Ingrid Skjoldvær

Ingrid Skjoldvær Alizaliwa tarehe 8 Agosti 1993 ni mtaalam wa mazingira wa Kiorwaya na mwenyekiti wa zamani wa shirika la mazingira la Nature and Youth. Anatokea Sortland katika eneo la Vesterålen na amekuwaakishikilia nafasi mbalimbali katika shirika hilo, hivi karibuni alikuwa ni makamu mwenyekiti, kabla ya kuchaguliwa kuwa kiongozi wa shirika tarehe 10 Januari 2016, nafasi ambayo alishikilia hadi 2017..[1] . Skjoldvær alihusika pia katika harakati dhidi ya mradi wa uchimbaji madini uliopangwa na Nordic Mining katika Fjord ya Førde mwezi Februari 2016.[2], amehusika sana pia katika harakati za Nature and Youth dhidi ya mafuta. Skjoldvær amefanya kazi katika taasisi ya mazingira ya Bellona kama mshauri mkuu wa mafuta,[1] na hapo awali alikuwa mwanachama wa Bodi ya Kitaifa ya Jamii ya Norway ya Uhifadhi wa Asili kuanzia 2015 hadi 2017.[3] Kwa sasa Skjoldvær ni Naibu Mwenyekiti wa Harakati ya Wananchi ya Oil Free Lofoten, Vesterålen, na Senja (Folkeaksjonen). Mwaka 2018, Nature and Youth waliungana na Greenpeace na Kampeni ya Hali ya Hewa ya Wazee kuwashtaki serikali ya Norway kwa kufungua maeneo mapya ya Aktiki kwa uchimbaji mafuta. Umoja wa makundi matatu ya mazingira ulidai kuwa hatua ya serikali ilikiuka Katiba ya Norway pamoja na ahadi ya taifa kwa Mkataba wa Paris.[4] Mahakama iliamua kuwa uchimbaji wa sasa na ule uliopendekezwa haukiuki haki ya kikatiba ya hali ya hewa bora.[5] Hata hivyo, mafanikio yalipatikana kwa Skjoldvær mwezi Aprili 2019, wakati harakati za Folkeaksjonen, pamoja na ushirikiano wake na mashirika mengine ya Norway na wanasiasa, yalisababisha ulinzi wa kudumu wa Lofoten, Vesterålen, na Senja dhidi ya uchimbaji mafuta.[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "Ingrid Skjoldvær". Natur og Ungdom. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 June 2015. Iliwekwa mnamo 5 May 2019.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  2. "Avviser klager mot sjødeponi". Putsj. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 May 2019. Iliwekwa mnamo 5 May 2019.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  3. "Ingrid Skjoldvær from Young Friends of the Earth Norway to speak at Arctic Frontiers 2017". MyNewsDesk. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 May 2019. Iliwekwa mnamo 5 May 2019.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  4. Neilza Polidore (22 November 2017). "The People vs Arctic Oil: Historic climate trial ends". Greenpeace.org.uk. Iliwekwa mnamo 19 May 2019.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  5. Thomas Nilsen (4 January 2018). "Environmentalists lose climate lawsuit over Arctic oil drilling". The Barents Observer. Iliwekwa mnamo 19 May 2019.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  6. "Labour Party of Norway Commits to Permanently Banning Oil Exploration in Norwegian Arctic". GlobalNewsWire. 4 April 2019. Iliwekwa mnamo 19 May 2019.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)

MAKALA YA PILI[hariri | hariri chanzo]

'Francisca "Paca" Blanco Díaz '

Francisca "Paca" Blanco Díaz ni mwanaharakati wa Kispanyola wa kike, mwanamazingira, mpinga ukandamizaji wa kifashisti, nguvu za nyuklia , ubepari na mstaafu. Blanco Díaz alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Ecologists in Action na ni sehemu ya Plataforma de Afectados por la Hipoteca, pamoja na wengine.

Wasifu wa Blanco Díaz

Francisca Blanco Díaz alizaliwa Madrid tarehe 13 Februari 1949. Baba yake alikuwa mfungwa wa kisiasa Mrepublikan aliyekuwa katika kambi ya mateso mpaka umauti ulipomfika. Baba yake alipofariki Blanco Díaz alikuwa na umri wa miaka 16. [1] alimaliza shule akiwa taari ni mama wa watoto wa watoto 5. [1] Kwa upande wake, maisha ni chuo kikuu kinachofundisha wale wanaotaka kujifunza na alisoma sana. Alipokuwa kijana, alisaka vitabu vilivyokatazwa vya Karl Marx, Leon Trosky, na Friedrich Engels. Alikisoma na kufikiria juu ya udhalimu wote ambao baba yake aliteseka, na yale aliyoyaona na kuteseka yeye mwenyewe katika shule za marekebisho. Uwezo wa kuunganisha alichokisoma na alichokiona karibu yake ni msingi wa utamaduni kwake. Ameishi katika miji kadhaa ya Hispania na amekuwa na maisha ya kazi "yasiyo ya kawaida" [2], akilazimika kufanya kazi kadiri awezavyo bila kujali ubora wa kazi kwa sababu alilazimika kuwatunza watoto wake. [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 "Paca Blanco: “Debo decir que nunca he tenido miedo, pero a veces he tenido que pedir protección”". www.elsaltodiario.com (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 2022-06-13. 
  2. Pérez-Lanzac, Carmen. "Un lugar protegido... ¡lo estará por algo!", El País, 2014-02-07. Retrieved on 2022-06-25. (es)