Mtumiaji:Jadnapac/Told Cities

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Told Cities Tanzania 2021 ni mradi unaolenga kuandika, kuhariri, kuboresha na kuongeza maudhui ya miji mikongwe nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na majengo yake ambayo kiujumla yanatambulika na shirika la UNESCO kuwa ni urithi wa Dunia. Mradi huu pia unahusisha kuhariri na kuongeza maelezo kwa Kiswahili katika mradi wa Wikidata kuhusu mada hii hii ya miji, majengo ya zamani nchini Tanzania pamoja na alama/nyumba mbalimbali za sanaa za kihistoria (museums). Mradi huu unafanyika Tanzania kwa kushirikiana na Kundi la wahariri wa Wikipedia hapa Tanzania na lile la Wiki World Heriatge User Group ambao ni kundi la watumiaji wanaojikita kuandikia zaidi mambo mbalimbali ya kihistoria ambayo kwa namna moja ama nyingine ni urithi kwa Ulimwengu. Hapa Tanzania mojawapo ya majengo mengi ya kale yanayotambulika na UNESCO yanapatikana katika mji mkongwe wa Zanzibar (Zanzibar Stone Town).

Shughuli za Mradi huu[hariri | hariri chanzo]

Wassiriki wa mradi huu wanataegemewa kufanya kazi kuu za aina mbili; Moja ni Uhariri/kutafsiri makala kutoka kiingereza kuja Kiswahili, kuboresha makala zilizopo kwa kuongeza picha, na kuhariri maelezo katika Wikidata. Pili ni wapiga picha kupakia picha mbalimbali za maeneo yoyote nchini Tanzania, picha hizo zinatakiwa kulenga majengo au majumba ya sanaa ya kihistoria ambayo kwa namna fulani huchukuliwa kama ni urithi wa nchi au Dunia kwa ujumla.


Orodha ya makala za kufanyia kazi[hariri | hariri chanzo]

Mradi huu unalenga kuongeza makala katika Wikipedia hii ya Kiswahili kuhusu maeneo/majengo mbalimbali ya kihistoria kama vile majengo yanayopatikana katika Kategoria ya Wikipedia ya Kiingereza na orodha nyingine itaongezwa hapo baadade.

Tuzo kwa Washiriki[hariri | hariri chanzo]

Mradi huu utatoa tuzo kwa washiriki hai kama ifuatavyo; 150USD, 100USD, na 50USD kwa wahariri bora watatu wa kwanza na 150USD, 100USD, na 50USD kwa wapiga picha bora watatu wa kwanza.