Mtumiaji:JLswahili123
Mipango Miji katika Kambodia
Muhtasari/Utanguilizi
Mipango miji katika Asia ya Kusini Mashariki inajulikana duniani. Kambodia inajulikana kwa mazingira ya asili na majengo ya kihistoria. Wakati wa utawala wa Khmer na ukoloni, ardhi ya nchi ilitumika kwa faida ya kikoloni na utawala wa Khmer. Uchumi wa Kambodia ulitegemea viwanda vya kilimo na nguo na utalii. Viwanda hivi vilisaidia uchumi wa Kambodia lakini mipango miji na maendeleo ina athari nzuri na mbaya.
Historia ya Mipango Miji
Mipango miji ilianza katika Asia ya Kusini Mashariki wakati wa zama za kale. Mipango miji iliunda uongozi wa kidini na taratibu katika nchi ya Kambodia. Kwa mfano, mipango miji ilionyeshwa katika miji takatifu katika nchi za Kambodia, Myanmar, na India. Mji mtakatifu katika Kambodia jina lake ni Angkor Wat. Kuna pia hekalu la Kipagani katika Myanmar na Bodh Gaya katika India. Mipango miji na ujenzi katika mji mtakatifu kama vile Angkor Wat iliunda mji mkuu na wilaya katika Kambodia.
Kazi ya Wafalme Watatu Maarufu
Wafalme watatu maarufu kutoka historia ya mipango miji katika Kamboja ni muhimu kwasababu wao walikuwa na athari ya kushawishi. Mmojawapo wa wafalme maarufu wa kwanza katika historia ya Kambodia jina lake ni Jayavarman wa pili. Yeye anajulikana kama mwanzilishi wa utawala wa Khmer kutoka mwaka 802 hadi mwaka 834. Wakati wa utawala wake, Jayavarman wa pili alianza utawala wa kifalme wa dunia sawa na dini ya kihindu[1]. Mafanikio ya Jayavarman wa pili yalisukumwa na utamaduni wa India.
Mfalme wa pili maarufu jina lake ni Suryavarman wa pili (Picha 1).
Yeye alitawala kutoka mwaka 1113 mpaka mwaka 1150. Alijulikana kwa kupanua wilaya katika Kambodia na aliunda uhusiano wa kidiplomasia pamoja na nchi jirani kama vile, China, Vietnam, Myanmar, Thailand na Malaysia. Pia Suryavarman wa pili alijulikana kwa ujenzi wa hekalu jina lake Angkor Wat (Picha 2).Angkor Wat ilijengwa kama heshima kwa Vishnu na iliunda mji mkuu. Huu ulikuwa mwanzo wa mipango miji na serikali na mifumo ya maji katika Kambodia. Angkor Wat ni muhimu kwa usanifu majengo, kidini, na utamaduni kwa kipindi hiki[2]. Sanaa iliyotengenezwa kwenye Angkor Wat inaonyesha historia ya nchi, ufalme, na dini. Mfalme wa tatu maarufu jina lake ni Jayavarman wa saba. Yeye alijulikana kwa ujenzi wa Bayon na Angkor Thom. Hekalu hili liliunda usawa na mfumo wa utetezi katika Bayon. Bayon ilichongwa kwa sura za nyuso kwenye hekalu (Picha 3).
Athari ya Ukoloni wa Wafaransa
Kambodia ilianguka baada ya mfalme Jayavarman wa saba. Kambodia ikawa koloni la Ufaransa katika mwaka 1863 hadi mwaka 1953. Katika kipindi hiki nchi nyingi katika Asia ya Kusini Mashariki zilikuwa na sehemu ya umoja wa Ufaransa. Pia katika wakati wa ukoloni wa kifaransa, mipango miji mipya, akiolojia, na shirika la kijamii ilianza. Hii ilisababisha kazi ya kurejesha mahekalu ya zamani na maendeleo ya mijini (Picha 4).Kambodia ilipata uhuru kutoka Ufaransa tarehe tisa mwezi Novemba mwaka 1953 lakini athari ya koloni la Ufaransa inaonekana katika mipango miji ya kisasa.
Mipango Miji ya Kisasa
Mipango miji ya kisasa ya Kambodia inaonesha kilimo, bidhaa za viwandani hasa katika mji mkuu Phnom Penh na mji maarfu Siem Reap. Mipango miji kwa mahekalu ya zamani kama Angkor Wat ilibadilisha mazingira ya mijini ya mji wa Siem Reap. Shirika la barabara na majengo linaonesha mipango miji ya Ufaransa. Maendeleo ya miji ni kwa hifadhi na utalii. Siem Reap ilikuwa na asilimia 28 ya hoteli na asilimia 71 ya nyumba za wageni[3]. Hoteli zilijengwa karibu na miji mikubwa kwa utalii.
Pia juhudi za utalii katika mipango miji ya kisasa zinatoa kipaumbele katika uhifadhi wa maeneo ya kihistoria. Mamlaka ya Apsara ambayo ilianzishwa mwaka 1995 katika Siem Reap ilisimamia uhifadhi wa kihistoria, utalii, na maendeleo katika wilaya ya Siem Reap. Mamlaka ya Apsara ilihifadhiwa katika Angkor Wat na Angkor Thom. Pia Mamlaka ya Apsara iliongoza mradi wa Spean Preah Toeus (Picha 5).
Spean Preah Toeus ni daraja nje ya kituo cha jiji katika nyakati za zamani. Marajesho ya daraja hili yanaonyesha uhusiano kati ya utamaduni na historia ya Kambodia. Marajesho haya ya mahekalu na tovuti zingine za kihistoria zilihifadhi utamaduni na zilitengeneza ukuaji wa uchumi kupitia utalii.
Mji mkuu wa Phnom Penh katika Kambodia unaonesha mabadiliko ya mipango miji. Lengo kuu la maendeleo ya miji ni kusaidia utamaduni na mazingira na kuhifadhi mji vizuri. Lakini ukuaji wa maendeleo zaidi katika miji unaweza kuwa mbaya. Kwa mfano katika mji mkuu wa Phnom Penh maendeleo ya majengo yameleta matatizo mengi. Pia idadi ya watu katika mji inategemea kuongezeka kwa asilimia 22.1 kwa mwaka 2020 (Picha 6).Phnom Penh ilikuwa na upungufu wa nyumba za bei nafuu kwasababu ya ukuaji wa uchumi na mipango miji[4]. Tatizo hili limesababisha kutokuwa na usawa katika mji kwasababu maendeleo ya miji hayasimamiwi. Maendeleo ya miji hayasimamiwi kwasababu utalii unaleta fedha nyingi katika nchi ya Kambodia.
- ↑ Hays, Jeffrey. “Khmer Dynasty and the Rulers of Angkor.” Southeast Asia, May 2014. Accessed 9 Apr. 2019
- ↑ World Heritage Convention. “Angkor.” United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO). Accessed Apr. 2019.
- ↑ Esposito, Adele. Urban Development in the Margins of a World Heritage Site: in the Shadows of Angkor. Amsterdam: Amsterdam University Press, 2018. Print.
- ↑ United Nations Population Fund. “Urbanization and its Linkage to Socio-Economic and Environmental Issues.” UNFPA Cambodia, 2014, pp. 1-40. Accessed Apr. 2019