Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Joeangatia/Semaglutide

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

 

Dawa ya Semaglutidi (Semaglutide) inayouzwa chini ya jina la chapa Ozempic miongoni mwa majina mengine, ni dawa inayotumika kutibu kisukari cha aina ya 2 na unene uliokithiri.[1] Haipendelewi zaidi kuliko dawa ya Metformini (Metformin), ingawa zinaweza kutumika pamoja.[1][2] Inaboresha udhibiti wa sukari ya damu, hupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo, na kupunguza hatari ya matatizo ya figo.[1] Dawa hii hutumiwa kupitia mdomoni au kwa kudungwa sindano chini ya ngozi.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, kutapika, kuhara, maumivu ya tumbo, na kufungika choo.[1] Madhara yake makubwa yanaweza kujumuisha ugonjwa wa ya kisukari wa mwili hutoa asidi nyingi za damu[3] (ketoacidosis), sukari ya chini ya damu, na kongosho.[2] Kuna wasiwasi kwamba matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto, na kuitumia wakati wa unyonyeshaji hakupendekezwi.[1] Dawa hii inafanya kazi kama glukagoni ya kibinadamu inayofanana na peptidi-1 (GLP-1), huongeza kutolewa kwa insulini, inapunguza kutolewa kwa glukagoni, na kupunguza uondoaji wa chakula tumboni.[2]

Semaglutidi iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2017.[1] Ilitengenezwa na Novo Nordisk [1] na ilikuwa GLP-1 ya kwanza ambayo inaweza kutumiwa kupitia mdomoni. Nchini Uingereza miligramu mbili za sindano hugharimu Huduma ya Taifa ya Afya (NHS) takriban £73 kufikia mnamo 2020.[2] Kiasi hiki nchini Marekani kinagharimu takriban dola 850 kufikia mnamo 2021.[4]

Marejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "Semaglutide Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). American Society of Health-System Pharmacists. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 2 Aprili 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "AHFS2021" defined multiple times with different content
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 BNF (tol. la 80). BMJ Group and the Pharmaceutical Press. Septemba 2020 – Machi 2021. uk. 738. ISBN 978-0-85711-369-6.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: date format (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "BNF80" defined multiple times with different content
  3. "Diabetic ketoacidosis - WikiProjectMed". mdwiki.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-08-31.
  4. "Ozempic Prices, Coupons & Savings Tips". GoodRx (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Septemba 2021. Iliwekwa mnamo 16 Aprili 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)