Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Godfrey .J. Ndyanabo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

GODFREY JUSTUS NDYANABO

Karibuni sana rafiki zangu tupate kuzungumza, kujadiliana na kubadilishana mawazo japo mawili matatu, utakaloona linafaa ruksa kulichukua na kulifanyia kazi na kwa lile litakaloonekana kuwa kinyume chake basi achana nalo. Awali ya yote ningependa kuchukua wasaa wako mchache kujitambulisha walau upate kunifahamu japo kwa ufupi.


UTAMBULISHO MFUPI

Majina yangu kamili ni Godfrey Justus Emily Ndyanabo, nilizaliwa mnamo tarehe 2 Februari miaka kadhaa iliyopita. Mimi ni mzawa wa mkoa wa Mwanza lakini asili yangu ni mkoa wa Kagera kwa maana ya kwamba wazazi wangu wote wawili ni wazawa wa mkoa wa Kagera hivyo basi itoshe kusema kabila langu ni mhaya.

Nilibahatika kupata elimu ya msingi katika shule ya Msingi Nyamanoro iliyoko katika wilaya ya Ilemela jijini Mwanza. Baada ya takribani miaka saba kwa mapenzi ya Mungu nilifanikiwa kuhitimu elimu ya msingi katika shule ya msingi Nyamanoro.

Kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu nilibahatika kujiunga na shule ya Sekondari Pamba iliyoko katikati ya Jiji la Mwanza katika wilaya ya Nyamagana. Baada ya kipindi cha takribani miaka minne nilifanikiwa kuhitimu elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Pamba.

Kwa kudra za Mwenyezi Mungu, nilibahatika kuchaguliwa kujiunga katika shule Sekondari ya wavulana ya Nsumba kwa ajili ya masomo ya kidato cha 5 na 6 kwa mchipuo wa PCM yaani FIZIKIA, KEMIA na HISABATI. Elimu hii katika shule ya Sekondari Nsumba ilitamatika rasmi baada ya kipindi cha miaka miwili.


MITANDAO YA KIJAMII

Kunako mitandao ya kijamii napatikana na unaweza kunifuata katika kurasa zangu kama ifuatavyo:

Twitter: @gody_ndyanabo

Instagram: @godfrey_ndyanabo

Facebook: Godfey Ndyanabo ama Godfrey Justus Ndyanabo