Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Efraim Malisa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Efraim Malisa ni mtoto wa tatu wa kuzaliwa kwenye familia ya Mzee Tertio Ndesamburo Malisa yenye watoto saba. Alizaliwa mwaka 1978 Kijiji cha Kidia, Kata ya Old Moshi wilaya Ya Moshi Vijijini, Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.

Efraim and Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Kilimo, Shahada ya Uzamili ya Maendeleo vijijini, na Cheti cha Menejiment katika uendeshaji wa Programu za Kilimo biashara. Pia amehudhuria kozi fupi fupi kwenye maswala ya Ufuatiliaji na Tathmini ya miradi, Tiba ya mifugo,Kilimo cha bustani n.k

Efraim ni mtaalamu wa maendeleo vijijini haswa kwenye uzalishaji na masoko.Ni mwalimu katika maswala ya kilimo endelevu.kilimo Biashara,Ufugaji bora wa  Kuku na Mbuzi,Uandishi wa miradi ya maendeleo, Tathmini ya uzalishaji na Mahesabu ya faida.

Efraim amefanya kazi na mashirika mbalimbali na kwa nafasi tofauti ikiwemo,Mratibu wa Mkoa kwenye Mtandao wa Vikundi vya wakulima Tanzania,Mtaalamu wa Kilimo Hifadhi-Care International, Mtaalamu wa Kilimo Endelevu-Care International(Morogoro),Kaimu Mratibu Miradi wa kumuinua Mkulima-Care International, Mratibu msaidizi na Msimamizi mkuu wa utekelaji-Care International. Pia amefananya kazi kama Mtafifi mwenza Fert Arusha, Mratibu wa kanda kwenye maradi wa Kilimo-Fert Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Shirika la vijana Arusha Voice Of Youth Tanzania,Kwa Sasa Ni Meneja wa program VOYOTAPia Mwezeshaji mwenza Kilcher Compony Limited-Inayohusika na Utafiti elekezi kwa Sector ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.

Pamoja na mambo yote hayo Efraim amekua akitumiwa na Mungu kwa nyakati mbali mbali ikiwemo,Mwenyeki wa UKWATA[1] Karatu Secondary, Mwenyeketi wa Ukwata Kanda ya Karatu, Mwenyekiti wa kamati ya uinjilisti USCF[2]- SUA, Mwenyekiti wa USCF-SUA-Mazimbu campas, Mwenyekiti wa USCF-SUA, Main,Mwenyekiti wa Campas zote-USCF-SUA na Mwenyekiti wa Uinjilisti- TAFES[3] Mkoa wa Morogoro. Pamoja na nafasi hizo amekua mwalimu na Mhubiri wa neon la Mungu kwa watu mbali mbali ikiwemo kupitia semina za ndani, Mikutano ya Hadhara,Vyuoni na Kwenye matukio mbali mbali ya maisha


[1] Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania

[2] United Students Christian Fellowship

[3] Tanzania Fellowship Of Students