Mtumiaji:Dexter Ghikas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hamjambo nyote! Najivunia mno kuwa miongoni mwa wanaoendeleza lugha hii tukufu ulimwenguni! Ahsanteni sana wasimamizi wa wikipedia kwa kutupa fursa hii ya kipekee kushirikiana pamoja kwa njia hii, nanyi wenzangu kwa kuuitikia mwito huu muhimu. Naitwa Dexter, natoka Kenya na ndio nchi yangu ya kuzaliwa. Hivi sasa niko katika mji mkuu wa Nairobi ambako naifanya kazi ya uhandisi kwa ujenzi wa nyumba, barabara na kadhalika. Natumai tutakuwa na wakati murwa na tutajifunza mengi na zaidi ya yote tutaiinua na kuiendeleza lugha yetu!!