Nenda kwa yaliyomo

Jeshi la Ulinzi la Israeli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mtumiaji:Dee Soulza/7)
Nembo ya Jeshi la Ulinzi la Israeli
Bendera ya Israeli na Nembo

Jeshi la Ulinzi la Israeli (kwa Kiingereza Israel Defense Forces, kifupi: IDF; Kiyahudi: צְבָא הַהֲגָנָה לְיִשְׂרָאֵל‎ ‎  Tsva ha-Hagana le-Yisra'el ?, kwa ufafanuzi wa neno kwa neno: Jeshi la Ulinzi wa Waisraeli, pia hutajwa kwa finyanzo la Kiebrania Tzahal (צה״ל), ni jeshi la ulinzi la taifa la Israeli.

IDF ni jeshi lenye sehemu kuu tatu: Jeshi la Askari wa Miguu la Israeli, Jeshi la Anga la Israeli na Jeshi la Wanamaji la Israeli.[1] Ndio tawi pekee la kijeshi la vikosi vya ulinzi na usalawa vya taifa la Israeli. IDF huongozwa na Mkuu wa Jeshi, ambaye huwa chini ya Waziri wa Ulinzi wa Israeli.

Chini ya maelekezo ya Waziri Mkuu wa kwanza David Ben-Gurion, IDF ilianzishwa mnamo tarehe 26 Mei 1948 na lilianza kwa kutumikisha watu kisheria , huku wasajiliwa wake wa awali kabisa wakiwa ni askari ambao tayari walikuwepo, wa kundi la kijeshi la Yishuv — maarufu kama Haganah, [Irgun], na kundi lingine lililojulikana kama Lehi. Lilianzishwa muda mfupi baada ya Israeli kujitangazia uhuru wake na limeshiriki katika kila mgogoro wa kivita ambamo Israeli ilihusika.

Ndani ya vipindi vya mikataba ya amani; kati ya Israeli na Misri wa 1979 na ule wa Israel na Jordan wa 1994, IDF ilifanya mabadiliko makubwa ya kimkakati. Hapo kabla, jeshi hilo lilikuwa likisambazwa kwenye maeneo mbalimbali ya mstari wa mbele —Lebanon na Syria upande wa kaskazini, Jordan na Iraq upande wa mashariki, na Misri upande wa kusini — IDF ikahamishia umakinifu wake kwenye maeneo inayoyakalia ya kusini mwa Lebanoni na kwenye kuzikalia kimabavu himaya za Palestina za Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi, ikijumuisha Yerusalemu ya Mashariki. Mnamo mwaka 2000, IDF iliondoka kusini mwa Lebanoni na mnamo 2005 iliondoka Gaza. Mizozo kati ya Israeli na makundi ya Kiislamu ya Gaza, hususan Hamas, imekuwa ikiendelea tangia wakati huo. Zaidi ya hayo, mgogoro mwingine uliotikisa ni ule wa Israel na Syria, ambao ulikuwa ukifukuta mara kwa mara tangu 2011, kutokana na hali tete ya Mashariki ya Kati inayosababishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Syria.

Tangu mwaka 1967, IDF imekuwa ikijenga uhusiano wa karibu wa masuala ya kiusalama na Marekani,[2] wakishirikiana pia katika masuala ya utafiti wa maendeleo, wakiweka juhudi za pamoja kwenye uundaji wa McDonnell Douglas F-15E Strike Eagle au F-15I na makombora ya kujilindia ya Arrow , miongoni mwa mambo mengine . Pia inashukiwa kuwa IDF imejitengenezea na inamiliki silaha za kinyuklia tangia mwaka 1967, ikiwa na vichwa vya silaza hizo kati ya 80 na 400.[3] IDF inazidhibiti himaya za Palestina zinazokaliwa kimabavu na Israeli kupitia ukandamizaji, ubaguzi uliorasmishwa na uporaji wa haki za binadamu (za Wapalestina) na unyanyasaji wa kikatili; mambo ambayo yamekumbana na ukosoji mkubwa kote duniani.[4][5]

  1. "The State: Israel Defense Forces (IDF)". Israel Ministry of Foreign Affairs. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 18 Agosti 2021. The IDF's three service branches (ground forces, air force, and navy) function under a unified command, headed by the Chief of the General Staff, with the rank of lieutenant-general, who is responsible to the minister of defence.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Mahler, Gregory S. (1990). Israel After Begin. SUNY Press. uk. 45. ISBN 978-0-7914-0367-9.
  3. There is a wide range of estimates as to the size of the Israeli nuclear arsenal. For a compiled list of estimates, see Avner Cohen, The Worst-Kept Secret: Israel's bargain with the Bomb (Columbia University Press, 2010), Table 1, page xxvii and page 82.
  4. "Israel, West Bank and Gaza". United States Department of State (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Machi 2024. Iliwekwa mnamo 2024-08-03.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Israel's apartheid against Palestinians: a cruel system of domination and a crime against humanity". Amnesty International (kwa Kiingereza). 2022-02-01. Iliwekwa mnamo 2024-08-03.